CILAO YAMBURUZA TENA MAHAKAMANI DPP NA AG YADAI KUKAA KIMYA NI KURUHUSU SHERIA YA HAKI ZA BINADAMU KUKIUKWA ,MAOMBI YA KESI KUSIKIZWA KESHO

Na Joseph Ngilisho Arusha 


Shirika la Uraia na Msaada wa Kisheria CILAO linakusudia kukata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama yaliyoipa ushindi  Jamhuri dhidi ya mlalamikaji Odero Charles Odero aliyekuwa akipinga mtuhumiwa kukamatwa na kufungulia mashtaka bila upelelezi kukamilika ,akidai  imejaa ukiukwaji wa haki za kibinadamu.


Aidha shirika hilo tayari limewasilisha maombi hayo ya kufungua shauri hilo nje ya muda yanayotarajiwa kusikilizwa  Novemba 2 mwaka huu katika mahakama Kuu ya Tanzania masijala ndogo ya Dar es salaam.


Akiongea na waandishi wa habari mlalamikaji ,Odero Charles Odero ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika la CILAO 

alisema mwaka 2021 alifungua  kesi ya kikatiba mahakama kuu ya Tanzania masjala  ya Tanga na baadaye ilihamishiwa masjala kuu ya Dar es salaam.


Alisema kesi hiyo namba 21/2021 Odero alimshitaki mwendesha mashtaka wa serikali Dpp na mwanasheria mkuu wa serikali AG, akipinga watuhumiwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka bila uchunguzi kukamilika akiiomba mahakama itamke kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa katiba .


"Sisi kama shirika tunalofanya kazi ya utetezi wa haki za binadamu tuliona kitendo cha Dpp kukamata na kufungulia watu mashtaka bila uchunguzi kukamilika ni  kitendo cha ukiukaji wa haki ya binadamu  "


Alisema disemba 19 mwaka 2022 mahakama kuu ya kikatiba chini ya majaji watatu jaji mfawidhi Ilvin Mgetta ,jaji Benhajj Shabaan Masoud na jaji  Edwin Kakolaki ilitoa uamuzi wa kesi hiyo kwa kutupa maombi ya mlalamikaji huku ikisisitiza kuwa mlalamikaji Odero Charles Odero hakuonesha ushahidi au kiapo chake kuhusu hayo matendo aliyokuwa akilalamikia.


"Baada ya kupokea hukumu hiyo tulikaa chini kwa muda tukitafakari na wataalamu wetu wa sheria ambao wametushauri tukate rufaa na tayari tumeanza mchakato huo na maombi yetu tumewasilisha na kesho Novemba  mbili  yatasikilizwa ili kutolewa maamuzi na kufungua kesi ya msingi"


Alisisitiza kuwa kimsingi kesi hiyo sio ya mleta maombi pekee bali inagusa umma na inapaswa kupewa uzito wa aina yake na tayari pande zote mbili zimeitwa na mahakama na zimekubaliana kwa pamoja kuwa Novemba mbili maamuzi ya maombi hayo yatasikikizwa.


Odero  ambaye ni mwanaharakati na mtetezi wa haki za jamii kupitia shirika hilo la CILAO alisema miongozo inayokinzana na haki za kibinadamu sio ya kufurahia kwa kuwa ina madhara na hivyo shirika lake limejipambanua kupigania kuwepo kwa mifumo bora.


"Kwa mfano mtu akikamatwa mwaka 2022 na kukaa mahabusu na kesi yake kuamuliwa mwaka 2025 utakuwa umemnyima haki zake za msingi ikiwemo kupata madhara ya kiuchumi na kinyumba ,hivyo utaratibu huo unakiuka haki za kibinadamu"


Ends...











Post a Comment

0 Comments