WAHITIMU LA SABA TUMAINI JUNIOR USIPIME, MDHIBITI UBORA AIFAGILIA SHULE ATAKA WAZAZI MBIOMBIO WAPELEKE WATOTO WAO,WANAFUNZI TUMAIN SENIOR NAO WARUSHA SATELLITE ANGANI

 Na Joseph Ngilisho, KARATU

Wanafunzi wa darasa la saba wametakiwa kujitahidi katika mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu elimu ya msingi ili kuwawezesha kuendelea na masomo ya sekondari. 

Wito huo umetolewa na mdhibiti mkuu wa ubora wa elimu wilayani Karatu Samson Mkonyi katika mahafali ya 13 ya shule yenye mchepuo wa kiingereza ya Tumaini Junior iliyopo wilayani humo Mkoani Arusha, ambapo wanafunzi 94 wamehitimu masomo yao.

Mkonyi amewaasa wahitimu 94 wa SHULE hiyo ambao wanatarajiwa kufanya mitihani yao katikati ya mwezi huu, kujichunga na kujiepusha na tabia hatarishi ambazo zitafanya wakatishe ndoto zao.


Aidha Mkonyi aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kufanikiwa kutumia fursa ya kuanzisha shule hiyo yenye mchepuo wa kiingereza katika eneo hilo ili kuwapatia elimu bora wanafunzi na hivyo kuepusha watoto hao kufuata elimu hiyo umbali mrefu.





Alisema kuwa uongozi wa  shule umefanikiwa Kwa kiasi Kikubwa kutoa watoto kitaaluma katika nchi hii licha ya changamoto nyingi.


Akiongelea kuanzishwa kwa shule ya tumaini Junior ,alisema ilianzishwa katika mazingira magumu katika nyumba ya  kuishi huku wakikutana na changamoto  nyingi lakini ndoto  haikufa hivyo alipongeza juhudi hizo kuona shule imezidi  kustawi na sasa inamajengo ya kisasa na wanafunzi zaidi ya 600.


Shule ya Tumaini Junior imetajwa kuwa Bora kutokana na utendaji wake kuwa mzuri ikiwamo wazazi kuikubali shule hiyo na kuwaandikisha kwa wingi kufuatia watoto kulelewa katika mazingira Bora.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi za Elimu za Tumaini Junior na Tumaini Senior high school Modest Bayo  alisema wakati serikali ikitarajia kufanya mabadiliko makubwa ya mitaala , shule hiyo imejipanga ipasavyo.

Aidha Bayo aliwapongeza wazazi Kwa kuiamini shule ya Tumain Junior ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaasa wazazi kuendelea  kuwaandikisha watoto wao.


Aliwaalika watanzania wenye watoto  waliohitimu shule za msingi,kutoka Kada mbalimbali kuwaandikisha kwa wingi watoto katika shule ya sekondari Tumaini senior kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia 


Pamoja na hilo aliwatoa hofu wanafunzi na wazazi juu ya ujio wa mtaala mpya kwani waalimu tayari walishajipanga hivyo amewasihi wazazi na walezi kuondoa hofu.



Alisema kuwa hivi Sasa wanafunzi wa darasa la 7 wanataraji kufanya mtihani maeneo mbalimbali hivyo aliwakaribisha kuwaandikisha watoto katika shule ya sekondari Tumaini Senior Kwa kidato Cha 5 kwani nafasi bado zipo hivyo wazazi wasisite kujiunga na Tumaini senior high school.


Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alijivunia wanafunzi wake wa Tumain Senior kufanikiwa kurusha Satellite angani kuonyesha utaalam wao na ikumbukwe kuwa kazi kubwa satellite ni kuangalia hali ya hewa, kutengeneza mawasiliano, na nchi yeyote yenye satellite yake ina maendeleo makubwa.


Ends....


Post a Comment

0 Comments