(VIDEO)MPUMILWA AIBUKIA UZINDUZI WA JENGO LA PAPU ,AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Katibu wa Siasa na Uenezi(CCM) katika wilaya ya Meru,Mkoani Arusha, Kennedy Mpumilwa amewataka wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake kutumia fursa za kibiashara katika Kitega uchumi cha jengo la Makao Makuu ya umoja wa Afrika (PAPU),kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.


Mpumilwa amebainisha hayo wakati akiongea na chombo hiki cha habari katika hafla za uzinduzi wa jengo hilo ulifanywa na Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania ,Samia Suluhu Hassan na kuhudhuliwa na viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

"Uwepo wa jengo hili kubwa katika mkoa wetu wa Arusha ni kielelezo cha ukuaji wa uchumi, kunatoa fursa mbalimbali kwa wananchi,kwanza kabisa linakuza utalii kupitia wageni mbalimbali wanao kuja kwa shughuli za PAPU" alisema na kuongeza  kuwa

"Wageni  wengi waliokuja hapa kwa shughuli za uzinduzi wa jengo hili ni wengi sana ,wamelala katika mahoteli yetu ,wamekula hotelini na kwa mama ntilie ,wametumia usafiri wetu kwa hiyo mzunguko wa fedha ni mkubwa sana"

Aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kutokana na fursa nyingi za maendeleo anazoziibua na kusisitiza kuwa watumie kitega uchumi hicho cha Papu kuimarisha biashara zao.



                                   


Ends.......

Post a Comment

0 Comments