Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Kampuni ya Tigo nchini Tanzania imewahakikishia watalii watakao kuwa wakitembelea maeneo ya vivutio vya utalii hapa nchini kupata huduma za kimtandano na mawasiliano.
Akiongea na waandishi wa habari katika Tamasha la siku tatu la Maasai Festival ambapo Tigo ni mdhamini wa tamasha hilo linalofanyika katika viwanja vya Ngarenaro jijini Arusha.
Meneja wa Tigo Pesa Kanda ya Arusha,Eric Sositenes alisema Tigo imejipanga kusapoti dhana ya serikali ya kuhamasisha utalii kwa kuunga mkono jitihada za rais Samia Suluhu kupitia filamu yake ya RoyalTour.
"Tumefikia hatua ya kudhamini Tamasha hili kubwa la Maasai Festival,lengo ni kutaka jamii pamoja na watu mbalimbali waweze kuelewa umuhimu wa utalii na umuhimu kutambua jamii ya kimasai na mila zao"
Akiongelea huduma zinazotolewa na Tigo,kupitia banda lao lililopo katika maonesho hayo,alisema tigo imekuja na huduma mbalimbali kama mkopo ya simu kwa kuwawezesha wananchi wenye kipato kidogo kuweza kumiliki simu janja kwa kulipa kiasi kidogo cha sh,1000 kila siku.
"Wito wetu kwa vijana ni kuendelea kutumia huduma za tigo ambazo kwa sasa hivi ni digital na sisi tigo Tuna toa huduma bora za Internet kuweza kurahisisha matumizi ya Internet ukizingatia kwamba dunia ya sasa ni utandawazi"
Ends..
0 Comments