Na Joseph Ngilisho,Arusha
Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo imeahidi kuendelea kusapoti jitihada za serikali katika kukuza utalii kupitia matamasha mbalimbali ya kitamaduni ili kuchochea uchumi wa taifa kupitia huduma zake za mawasiliano zilizoenea kote nchini
Hayo yameelezwa na meneja wa Tigo Kanda ya Arusha ,Daniel Mainoya katika ufunguzi wa Tamasha la Maasai Festival linalofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro ambapo Tigo ni mmoja ya wadhamini wa Tamasha hilo la siku tatu.
Alisema kwamba Tigo inatambua umuhimu wa tamasha hilo na hawawezi kubaki nyuma lazima tuwe sehemu ya kuchochea utalii wetu kama chanzo cha mapato ya taifa.
Alisema Tamasha hilo la utamaduni wa Maasai limelenga kukuza Utamaduni na kutangaza vivutio mbalimbali vya asili zikiwemo tamaduni za kimaasai na wao kama kampuni ya kidigitali watahikikishha wanatoa huduma za mawasiliano maeneo yote ya utalii.
"Kama mnavyojua wageni wanapokuja kutoka nje wanatumia huduma za Internet kwa ajili ya mawasiliano na sisi Tigo tupo hapa kuhakikisha Tunawawezesha ili waweze kuwahudumia wateja wao "
"Tupo hapa katika viwanja vya Ngarenaro kuwaletea huduma zetu ambazo zinaweza kusaidia katika kukuza mawasiliano na wateja wakitembelea watakutana na huduma zetu zikiwemo simu janja ,kusajiri line na kurudisha line zilizopotea"
Alisisitiza kuwa kwenye Tamasha hilo wamekuja na huduma mbalimbali katika Banda lao Kwa siku zote tatu Kwa ajili ya Kutoa huduma Kwa jamii ikiwemo kutoa majawabu ya changamoto za malipo kama lipa Kwa Tigo pesa Kwa kutumia lipa namba lakini pia huduma za data.
Alisema kwamba wataendelea kuunga Juhudi za Serikali yetu ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kukuza Utalii wa Utamaduni sanjari na Utalii nchini Kwa kuendelea kudhamini Tamasha hilo na kwenye Tamasha hilo wamekuja na bidhaa kadhaa zipatikanazo kwenye kampuni hiyo.
Awali katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha,David Lyamongi
aliwataka viongozi wa kijamii na Machifu kuendelea kudumisha misingi ya Mila sanjari na kutunza Amani mshikamano na Umoja wa Watanzania.
Lyamongi aliyesema hayo wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo linanalofanyika kwa siku tatu kuanzia septembe 8-10 mwaka huu ,Jijini Arusha.
Alisema Tamasha la Wamaasai ni nguzo muhimu ya kuendeleza mshikamano na Umoja kupitia tamaduni zao sanjari na kukuza utalii wa Utamaduni nchini ili kuvutia wageni .
“Niwaombe viongozi wa Mila zetu kujenga misingi ya Maendeleo ya tamaduni zetu Ili kuendelea kuvutia utalii huu wa Utamaduni baada ya wageni kutembelea vivutio vyetu wapate muda wa kuendelea kuwepo nchini na hivyo kuongeza mapato yetu na taifa”
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Tamasha hilo la Maasai Festival Saitabau Nkemwa alisema Tamasha hilo lilianzishwa Kwa lengo la kutangaza Utalii wa kiutamaduni.
Alisema wameanza na kabila la Wamaasai Kwa Sababu ndilo kabila pekee lililodumu kwenye Tamaduni zake hadi Leo sanjari na kuunga Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan baada ya filamu ya Royal Tour kufungua utalii nchini.
Ends....
0 Comments