TAZAMA PICHA >MAJAMBAZI WATIKISA ARUSHA WAPORA MILION 30 SAA 2 USIKU ,WAMTEKA MKE NA WATOTO WAWAVUA DHAHABU ZA MILIONI 15,TAJIRI ALITOKA KUUZA GARI ,WALINZI WATOWEKA NA MAJAMBAZI

 Na Joseph Ngilisho Arusha 


Watu 7 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  wakiwa  na silaha za moto wamefunika nyuso zao , wakishirikiana na walinzi wa eneo la tukio ,wamevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Predators Safari Club na Arusha Water Drilling,Yusuph Khan  na kupora kiasi cha sh milioni 30 na vidani vya dhahabu vyenye thamani ya sh 15 milioni.

Picha za walinzi wa kampuni ya Wengwe 

Tukio hilo,limetokea Septemba 10 mwaka huu majira ya saa 2 usiku katika eneo la Kiranyi Sakina, wilayani Arumeru, baada ya majambazi hayo kumvamia Mkurugenzi huyo na kumweka chini ya ulinzi huku wakimpiga na  vitu vigumu .

Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo

Akizungumzia tukio hilo  Mkurugenzi Khan alisema majambazi hayo, kabla ya kufanya uporaji huo, yalifunguliwa lango la kuingia ndani na walinzi wake kutoka  kampuni binafisi ya Wengwe na walipoingia ndani waliwapiga na kumweka chini ya ulinzi yeye na familia yake ikiwemo kuwavua vidani vya thahabu watoto na mke wake.

"Nilikuwa na familia yangu  ndani na ndipo nilivamiwa na majambazi haya ambayo yalikuwa na silaha mbali mbali na kunijeruhi kisha kuingia ndani na kuchukuwa fedha na vito vya thamani baada ya kuwaweka chini ya ulinzi familia yangu "alisema

Aliwataja walinzi waliokuwa zamu kuwa ni,Moses Alfred Mabula (46) na Lazaro Richard Pruza(37) wote wakazi wa eneo la Daraja mbili jijini Arusha ambao kwa sasa wanasakwa na polisi juu ya tukio hilo.

"Kamera za usalama zinaonesha walinzi ndio waliwafungulia mlango majambazi na kuingia ndani kupora na baada ya hapo wamekimbia na hawajulikani walipo"alisema

Khan aliomba Jeshi la Polisi na Serikali kusaidia kukamatwa walinzi na majambazi hao, kwani fedha zilizoporwa alikuwa amepokea jumamosi jioni baada ya kuuza gari yake aina Mitsubishi Canter yenye namba za usajili T196 DRX .

"Baada ya tukio tulitoa taarifa polisi ambao walifika na kuanza uchunguzi na tayari kesi imefunguliwa"alisema

Meneja wa kampuni ya predators Safaris  Club Ltd , Stive laizer alisema kampuni hiyo, itatoa zawadi ya sh 2 milioni mbili kwa ambao atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao hawa walinzi.

"Hili ni tukio la kupangwa sasa ambao atawezesha kukamatwa na polisi walinzi waliotoweka tutatoa zawadi ya sh  milioni mbili"alisema

Mmoja ya shuhuda wa tukio hilo Julius Manase mkazi wa Kiranyi alisema, walipata taarifa ya tukio hilo baada ya kuona kikundi cha watu wakikimbia usiku kutoka katika nyumba hiyo ambapo pia kuna Karakana ya magari.

"Huu ni wizi wa kupanga tunaimani watuhumiwa watapatikana kwani Arusha, tulianza kusahau matukio ya aina hii lakini sasa yameanza kurudi"alisema.

Meneja wa kampuni ya ulinzi ya Wengwe ,Juma Masuka alithibitisha kuwa walinzi hao wanatoka kampuni yake na sasa wanashirikiana na jeshi la polisi kuwasaka popote walipo na alitoa wito kwa wananchi kusaidia  kukamatwa kwa walinzi wake wanaohusishwa na ujambazi

Ends.. 

Post a Comment

0 Comments