TAZAMA PICHA 20 BORA VIBE LA MWAKA MMOJA ARUSHA LIVE,MKURUGENZI AANGUSHA NG'OMBE KUWASHUKURU WATEJA, NI BAR INAYOBAMBA ARUSHA NZIMA, ATAKA KALOLENI ITANGAZWE ENEO LA STAREHE .

By Ngilisho TV Arusha

Ukiulizwa ni maeneo gani ya starehe yanayobamba katika jiji la Arusha, bila shaka hutaacha kutaja jina la ARUSHA LIVE iliyopo kaloleni hakika wameheshimisha jiji la Arusha kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali pamoja na wageni wanaokuja kwa shughuli za utalii.

FREDY MAIMU ni mkurugenzi wa ARUSHA LIVE ameiomba serikali ya mkoa kulitangaza eneo la Kaloleni kuwa ni eneo salama la Starehe kwa wageni mbalimbali wanafika jjjini Arusha. 

ARUSHA LIVE jana September 17 2023,imetimiza mwaka mmoja wa kutoa huduma bora ya vinywaji, vyakula na burudani tangia kuanzishwa kwake mwaka jana bila kutetereka ni jambo la kujivunia hasa kipindi hiki kuna ushindani mkubwa wa kibiashara.

Mkurugenzi wa MAIMU alisema anajivunia kufikisha mwaka mmoja tangia kuzinduliwa kwa Bar hiyo inayobamba  jijini Arusha na kuwashukuru wateja wake ambao wameendelea kumuunga mkono na kueleza kuwa mambo mazito zaidi watarajie.

Katika hafla hiyo ya kusherehekea mwaka mmoja wa ARUSHA LIVE burudani ya kukata na shoka iliangushwa huku uongozi wa ARUSHA LIVE ukiangusha Ng'ombe mzima kuwashukuru wateja wake ambao walikula na kunywa bureeeeeeeee.







 



 

















Post a Comment

0 Comments