RC MONGELA AWASHUKIA VIKALI MA-DC NA MA -DED ARUSHA"MSIFIKIRI NIMEZEEKA NINYI NDIYO MNANIZEESHA'

Na Joseph Ngilisho Arusha 

MKUU wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha miradi yote ya maendeleo vikiwemo vipolo inayotekelezwa katika mkoa huo inakakamilishwa kulingana na ratiba ya miradi hiyo kabla ya mwaka huu kumalizika .

Agizo hilo amelitoa Septemba 4 alipokuwa akifungua kikao kazi cha kutathimini ya ukamilishaji wa miradi kilichoshirikisha ,Sekretarieti ya mkoa,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,Wakuu wa Wilaya,makatibu Tawala wa Wilaya

Wengine ni wenye Viti wa halmashauri,Wakurugenzi watendaji wa halmashauri, Wakuu wa Idara ,za halmashauri, Wakuu wa Wakala wa Taasisi za Serikali ,Wakuu wa manunuzi na Maafisa mipango kilichofanyika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa.

Mongela,alisisitiza Kila mmoja kuhakikisha usimizi na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwenye Wilaya yake Katika mkoa huo lengo ni kuwezesha Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuifuatilia kwa ukaribu zaidi .

Alisema kila Wilaya itakabidhiwa Kabrasha la miradi inayotakiwa kutekeleza ndani ya mwaka kwa kuwa Kila mradi umeletewa fedha hivyo wahakikishe inakamilika na Kila Wilaya imesha pewa dediline ya utekelezaji wa miradi ipo ambayo inatakiwa kukamilika Septemba 31 Oktoba 31 na Desemba 31 mwaka huu hivyo hategemeibkuna mwaka unakwisha na mradi haujakamilika.

Aliwaambia kwamba kikao hicho kinatokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia,alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita ya Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wa mikoa yaliyohusu usimamizi na utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/23 ya miradi ndani ya wakati  yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani ,wiki iliyopita.

Alisema kuwa wakati Rais akifunga mafunzo hayo ametoa maelekezo Kwa mikoa yote Nchini kuhusu usimamizi huo na amewaita Viongozi hao ili kuhakikisha maelekezo hayo hayabakii kwa Viongozi wa ngazi za juu pekee bali yaende hadi ngazi za kata hivyo kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kabla ya Desemba 31 mwaka huu.

Alisema kuwa haoni Kwa nini miradi hiyo isikamilike kwa kuwa Serikali kuu imetoa fedha zote za mradi husikana hivyo Kila Wilaya imepewa deadline ya kutekeleza miradi na fedha zipo na hakuna fedha za nyongeza kwa ajili ya miradi hiyo.

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Rea,Tanesco,Barabara,Maji  ,Ujenzi wa Vyumba vya madarasa,Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya afya n.k.

Alisema wanaokwamisha miradi mingi kukamilika kwa wakati ni Maafisa manunuzi pamoja na Maafisa mipango,ambao wamekuwa wakikwamisha miradi hiyo hivyo akawataka wabadilike

Alisema maeneo ambako miradi  imechelewa kukamilika ni yale ambayo  wataalamu wengi wamepiga kambi wakati maeneo ambayo hayana wataalu miradi inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kwa muda .

Aliwataka Viongozi wa Wilaya na halmashauri Kwa pamoja kushirikiana kuunda timu zitakazohusika na utekelezaji wa miradi kwenye ngazi za kata na akatahadharisha wasichaguliwe watu kwa vyeo vyao bali uwezo wao ndio wawe wajumbe wa Kamati.

Alizitaka halmashauri kugatua madaraka ya usimamizi wa miradi na kuyapeleka kwenye kata ambako ndiko miradi inatekelezwa .

Alisema kwenye manunuzi kumekuwepo na udanganyifu kwenye( Mateleo) malighafi za vifaa vya Ujenzi ambapo wamekuwa wakidanganya kwamba wananunua malighafi kwa bei ya Viwandani wakati wananunua Kwa mawakala.

Aliitaka halmashauri ziwe zinajadili taarifa za ununuzi na utekelezaji wa miradi sanjari na Wakurugenzi hukakikisha  wanatumia mifumo ya manunuzi  iliyopo kwenye halmashauri .

Ends...

Post a Comment

0 Comments