NG'ANZI HATAKI UTANI AFUNGIA SHULE 124 ZA UDEREVA NCHINI ,ADAI ZIMEKOSA SIFA ,AKIFAGILIA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KWA KUENDESHA MAFUNZO YA UDEREVA KWA VIWANGO

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani limezifungia shule 124 za udereva ambazo zilikosa sifa kutokana na uendeshaji mbovu, idadi ambayo ni sawa na asilimia 60 ya shule zote 130  ambapo kwa sasa shule 106 ndiyo zimekidhi vigezo na zina sifa na  zinaendelea kutoa kutoa mafunzo.

Aidha jeshi hilo limekipongeza chuo cha Ufundi Arusha, (ATC) kwa juhudi zake katika kuzalisha walimu wa udereva wenye sifa na vigezo vinavyokubalika ili kukabiliana na changamoto ya ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa jeshi la polisi nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi 
,Ramadhani Ng'anzi wakati alipotembelea chuo cha ufundi Arusha kinachotoa huduma ya mafunzo ya udereva.

Ng'anzi alifafanua kwamba sababu ya kufunga shule hizo ni pamoja na shule kukosa mfumo mzuri wa mazingira ya kujifunzia na  kufundishia ikiwemo baadhi ya shule kuzungukwa na maduka ya biashara.

Alisema sababu nyingine ni magari ya kujifunzia kutokaguliwa , shule kukosa vifaa."Tumezifungia na tukawapa miezi mitatu watengeneze miundombinu ya kufundishia wakishindwa hivyo tutawapokonya leseni,".

Alisema kuwa  asilimia 80 ya ajali zinazotokea hapa nchini  chanzo ni uzembe wa madereva na huwa wanatengenezwa kwa kuandaliwa katika vyuo vinavyotambulika.

Alisema chuo cha Ufundi Arusha kimepewa hadhi ya kuandaa madereva wa ngazi mbalimbali kuanzia leseni ndogo mpaka leseni ya juu ambapo hivi karibu polisi walihakiki madereva wa daraja C wawe wanaendesha mabasi ya umma na daraja E wanaoendesha magari ya mizigo.

ATC wameamua kushiriki  zoezi la mapambano ya kuondokana na ajali za uzembe wa madereva kwa kushirikiana na mawakala wao kwa kuzalisha walimu wa kutosha wenye sifa na vigezo vinavyokubalika.Sisi tunataka kuona viwango vya ufundishaji vinasambaa kutoka hapa kwenye shina (ATC) mpaka kwa mawakala wao kote nchini,".

"Tunaamini vitu vyote tulivyoona hapa ATC vifaa vya kufundishia michoro na alama za barabarani tutaenda kuvikuta kwa mawakala walio chini ya ATC. Wakala ambaye hatakidhi vigezo na masharti vilivyowekwa hatutasita kumfutia leseni,".

Kwa upande wao mawakala hao wa ATC akiwemo, Mkurugenzi wa Future world driving school ya jijini Dar es Salaam, Mkola alisema wao kama mawakala wanafahamu changamoto ziizopo kwenye fani hiyo ikiwemo ukosefu wa shule za udereva kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.

"Mnafahamu wingi wa magari tuliyonayo na uchache wa vyuo vya udereva tulio nao. Kuna wilaya na mikoa haina kabisa shule hizi na kwenye magari ya abiria na mizigo huko ndiyo kuna uhaba mkubwa na hivyo jitihada zinatakiwa ili elimu wa udereva iweze kuwafikia" alisema Mkola. 

Kwa upande wake mkurugenzi wa shule  St Brian Driving School, Robert Mwinje, amepongeza wekezaji mkubwa wa fedha uiofanyika na serikali kwenye chuo cha Ufundi cha Arusha.

"Tumeona ujenzi wa mabweni ya kisasa, hospitali inayojengwa kwa ajili ya kumaliza changamoto ya huduma za afya ndani ya jamii ya wanaATC na tumeona maabara kwa ajili ya magari ya kisasa yale yanayotengenezwa nchini na yale yanayoagizwa nje ya nchi," Mwinje ameeleza na kufafanua zaidi.

Ends.. 




Post a Comment

0 Comments