(PICHA)MWENYEKITI WA MTAA ARUSHA,AFUNGA OFISI ATOWEKA NA FUNGUO NA MHURI,ASAKWA NA POLISI ,WANANCHI WAMSULUBU HATUMTAKI NI MWIZI, DIWANI ACHARUKA AITA POLISI IMSAKE.

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Wananchi katika mtaa wa Ally Nyanya kata ya daraja mbili jijini Arusha ,wamemkataa kaimu mwenyekiti wa mtaa huo ,Kafimbi juma wakidai amekithiri kuwaomba rushwa pindi wanapohitaji huduma za  kugongewa mhuri ofisini.

Kufuatia madai hayo uongozi wa kata hiyo ukiongozwa na mtendaji wa kata  ,John Joseph umemvua madarakani Kafimbi juma na kumteua Clementi Mahimbo kukaimu nafasi hiyo na kuagiza jeshi la polisi limsake popote alipo ili arejeshe mhuri aliotoweka nao pamoja na funguo za ofisi.
Tukio hilo limekuja kutokana na wananchi kuchoshwa na mwenendo wa matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa Kaimu mwenyekiti huyo na kusababisha wananchi  wakose huduma muhimu katika kipindi cha muda  mchache aliohudumu katika ofisi hiyo. 

Kafimbi ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa ,alikaimishwa nafasi hiyo miezi miwili iliyopita kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa huo,Omari Shee ambaye yupo nje ya ofisi kutokana na matatizo ya kifamilia.
John Joseph afisa Mtendaji ,Daraja Mbili 
Jengo la kisasa la ofisi ya SERIKALI ya mtaa wa Ally Nyanya ,Daraja mbili ARUSHA
Prosper Msofe(Kushoto) Diwani Daraja mbili ARUSHA 
Akiongea katika mkutano wa hadhara aliouitisha mtaa hapo mtendaji wa kata hiyo ,John Joseph alidai kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakimtuhimu kaimu mwenyekiti huyo kuwaomba rushwa wanapokwenda kutaka huduma za kiofisi.
Mtendaji alieleza kuwa Kafimbi ameigeuza ofisi hiyo kuwa mali yake kwa kuwatoza wananchi fedha pindi wanapohitaji huduma za kiofisi,kupitisha barua za mikopo bila kufuata taratibu,kuomba rushwa pamoja na kutembea na mhuri wa ofisi kinyume cha sheria. 

Mtendaji huyo alilazimika kuitisha mkutano  huo uliohudhuliwa pia na diwani wa kata hiyo Prosper Msofe pamoja na viongozi mbalimbali wa kata, uliofanyika mtaani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari polisi ambapo wananchi walitoa kero mbalimbali huku malalamiko mengi yakielekezwa kwa Kafimbi. 
Baada ya malalamiko hayo afisa mtendaji  huyo alitangaza kumvua madaraka na kumteua, Clementi Mahimbo kukaimu nafasi hiyo na aliagiza jeshi la polisi kumsaka Kafimbi Juma popote alipo ili aje kujibu tuhuma zinazomkabili na kwamba iwapo itathibitika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kabla ya hatua hiyo Kafimbi alitoweka ofisini hapo na kufunga ofisi hiyo kwa zaidi ya wiki moja na aliondoka na mhuri wa ofisi pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi na hivyo shughuli za ofisi  kusimama na wananchi kukosa huduma.

Miongoni mwa wananchi waliotoa kero zao ni pamoja na ,Charles Olongo ambaye alisema  kuwa Kafimbi alikuwa akiwatoza sh,5000 ili kupata huduma ya kugongewa mhuri,pia alikuwa akikusanya fedha za ulinzi  wakati hakuna huduma hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Prosper Msofe alisema kuwa mtaa wa Ally Nyanya umegubikwa na matukio mengi ya uhalifu kutokana na kukosa uongozi madhubuti wa kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Diwani huyo alimtaja kafimbi kama kiongozi asiye na weledi na alikuwa sehemu ya wahalifu kutokana na tabia yake ya kuomba rushwa ,uchonganishi na kutoelewana na viongozi wenzake. 

Diwani huyo aliwapongeza wananchi wa mtaa huo kwa ujasiri wa kueleza tuhuma zake hadharani wakidai alikuwa tatizo katika ofisi ya mtaa  huobna wametoa maelekezo kwa jeshi la polisi kumsaka popote alipo ili aje kujibu tuhuma zinazomkabili na arejeshe  mhuri wa ofisi  aliotoweka kinyume na utaratibu.

Msofe alisema kuwa uwepo wa Kafimbi katika ofisi hiyo kumesababisha migogoro mingi isiyokoma ,uchonganishi na alikuwa kinara wa kuomba rushwa.

Ends...






Post a Comment

0 Comments