MWENYEKITI WA HALMASHAURI MONDULI JOSEPH KADOGOO MATATANI ,MKUU WA MKOA AMBURUTA MAHAKAMANI ATAKA KULIPWA MILIONI 200 KWA KUMTUSI,AJIKAANGA MAHAKAMANI

 Na Joseph Ngilisho Arusha

ALIYEKUWA mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Erasto Sanare amemfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isaac Joseph (Kadogoo) (45) akimtuhumu kumkashfu na kumtolea matusi mazito akitaka alipwe sh,milioni 200. 

Kagodoo amepanda mahakamani kujitetea kwenye kesi hiyo ya madai inayosikilizwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha. 

Sanare ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) mkoani Arusha anaomba kulipwa fidia ya shilingi milioni 200  kwa madhara aliyopata kutokana na maneno ya kashfa anayodai yalitolewa na Isaac dhidi yake.

Shauri hilo la madai namba 23/2022  linasikilizwa na hakimu mkazi, Aisha Ndossy wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo Sanare anawakilishwa na mawakili,  Kapimpiti Mgalula na Judith Reuben huku Isaac akiwakilishwa na mawakili Peres Parpai, Sendeu Nicolas na Yonas Masiaya.

Isaac anadaiwa kutoa maneno hayo Novemba 7,2022 akiwa Sinoni wilayani Monduli akiwa na watu wengine pamoja na waandishi wa habari ambapo anadaiwa kusema "ndugu yangu Sanare amejiongezea eka moja na pointi kwenye eneo ambalo hajapewa..huu ni wizi  imekuwa mambo ya kujirudiarudia sana kwa kiongozi huyu,".
 
Akitoa utetezi  wake  Agosti 31,2023,  Isaac ameieleza mahakama kuwa hajui kama Sanare aliwahi kuwa kiongozi zaidi anamfahamu kama mwananchi wa kawaida.

Akiongozwa na mawakili wake, mwenyekiti huyo wa halmashauri ya wilaya ya Monduli amesama kuwa akiwa kwenye eneo la mgogoro linalomilikiwa na taasisi ya Nanina ambayo Sanare ni mkurugenzi wake alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo aiandikie barua taasisi hiyo isitishe kufanya maendeleo yoyote kwenye eneo hilo.

Amedai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya yeye na  timu aliyokuwa nayo ambao walielekezwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Mwaisumbe kupima eneo hilo kujiridhisha kuwa taasisi ya Nanina imejiongezea eneo kama malalamiko ya wananchi na diwani wa eneo hilo, Nelson Lowassa.

"Siku hiyo hapakuwa na wananchi ni wataalam, eneo la mgogoro upande mmoja eneo la Nanina na upande mwingine ni eneo la halmashauri," amesema Isaac na kuongeza

....Sikuwa na chombo cha habari kwenye eneo hilo kwani ili kitambulike lazima awe amesajiliwa. Mlalamikaji kwa sasa ni mwananchi wa kawaida sijui kama ni kiongozi wa Mila," 

Hata hivyo Isaac akihojiwa na wakili Judith amesema hapakuwa na mwananchi wa eneo hilo wakati walipoenda kulipima wala hakuna mwananchi aliyefika mahakamani hapo kutoa ushahidi juu ya malalamiko hayo.

Mawakili wa Isaac walisema kuwa wamekamilisha ushahidi wao ambapo wameleta mashahidi watatu akiwemo diwani wa kata ya Engutoto na Afisa ardhi mteule wilaya ya monduli, Waziri Juma Hatibu 

 Hakimu mkazi, Ndossi ameahirisha shauri hilo mpaka septemba 15, 2023 majira ya saa 3 asubuhi kwa ajili ya kutoa uamuzi ambapo amewaagiza mawakili wa pande zote kuwasilisha hoja za majumuisho Septemba 13, 2023.

Awali akiongozwa na wakili wake Parpai Osaac ,aliieleza mahakama kuwa mbali ya uenyekiti wa halmashauri lakini pia ni mkandarasi.

Akaeleza kuwa majukumu yake kama mwenyekiti wa halmashauri ni kusimamia baraza la madiwani , kukagua wa shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi 

Isaac akaeleza kuwa eneo walilompa Nanona lilikuwa na ekari 10 hivyo baada ya kumpa Nanina ekari tano zilibaki tano ni za halmashauri ya Monduli. 

Ameendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa mnamo novemba 7,2022 majira ya saa tatu asubuhi aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumba alimuita ofisini kwake na kumuagiza afuatilie kero ya mgogoro wa ardhi.

" Nilipofika ofisini kwa DC ofisini nikawakuta wataalam wa ardhi na taasisi nyingine TAKUKURU na polisi. DC wa wakati huo alinieleza kero aliyosema ni ya muda mrefu tukajiridhishe juu ya kero ya eneo tuliyoipa taasisi ya Nanina iliyopo Sinoni kata ya Engutoto," ameeleza Isaac na kuongeza.

...Tuliondoka kwenda eneo linalolalamikiwa nikiongozana na watu Hao tukafika kwenye eneo hilo tukakuta Kuna maeneo yamewekwa uzio na lingine limejengwa kisima," 

"Tulipofika tulihakiki eneo alilopewa Nanina je limeingia eneo lingine tukiwa na wataalam tukakuta limeingia eneo ambalo hatukuwapa,".

"Mkurugenzi wa Nanina hakuwepo wakati upimaji ulifanyika. Baada ya kupima nikatoa maelekezo kwa DED amuandikia barua Mkurugenzi wa Nanina asitishe maendelezo mpaka baraza  tutakapokaa kuangalia,".

Isaac akaendelea kujitetea mahakamani hapo kuwa 
"Niseme sijamchafua Sanare nilikuwa naelekeza watu wowote wenye ardhi Monduli asijiongezee ardhi bila kufuata utaratibu akijiongezea huo ni wizi," amesema Isaac na kuongeza

...Sikutaja jina la mtu ila nilielekeza kwa watumishi kuwa kitendo hiki mtu akifanya huo ni wizi...Nikitembelea miradi nikikuta kuna uzembe sementi au vifaa huwa nasema  huu upotevu ni wizi. Wizi ni pale mtu anapochukua kitu ambacho hakupewa,".

Ends..

Post a Comment

0 Comments