Na Joseph Ngilisho Arusha
Akina dada wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo ya kaloleni jijini Arusha hususani katika eneo maarufu la Shivaz wamevamia kanisa la nabii Geordavie lililopo Kisongo na kumtaka awapatie mitaji ili waachane na biashara ya ukahaba.
Wakiongea mbele ya Nabii huyo na kumfanya atokwe na machozi ya uchungu walidai kuwa wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu kutokana na ugumu wa maisha .
Aidha walimweleza changamoto mbalimbali wanazopitia kwenye kazi yao ikiwemo kupigwa ,kurushwa ujira wao, kufedheheshwa kwa kutukanwa mtaani.
Walimweleza pia kuwa miongoni mwao wamo machangudoa wachungaji na kwamba iwapo atawapatia mtaji wataachana na biashara hiyo ya kuuza miili yao na kufanyakazi halali ya kujipatia kipato.
"Baba tunafanya hizi kazi KWA ajili ya kusomesha WATOTO tunamaisha MAGUMU sana tungepata mtaji tungeachana na hii biashara tunaomba utusaidie mitaji tunateseka sana baba kuuza miili yetu"
"Ukiitwa unaenda unafanya halafu hakulipi hela tunapitia MAGUMU sana katika hii kazi tunapigwa na tunatishiwa kwa bastola ,mtaani tunadhalilishwa tunaitwa Malaya na wengi wanaojiuza NI watumishi wa MUNGU waimbaji"
Nabii Geordavie baada ya kuwasikiliza aliahidi kuwasaidia kuwapatia mitaji .Aliwaombea waachane na biashara ya kujiuza.
Ends......
0 Comments