KISHINDO CHA RAIS SAMIA ,AZINDUA JENGO LA KIMATAIFA NI MAKAO MAKUU YA PAPU AFRIKA,NAPE : NI ALAMA KWA UMOJA HUO,TCRA WAHAMIA CHAP

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka Umoja wa Posta Afrika (PAPU)kupanua wigo wa kusafirisha vifurushi kwa kutumia mashirika ya ndege ya Afrika ili kuendelea kuonesha umuhimu wa kutumia huduma za posta barani humo.


Rais,ametoa Rai hiyo alipokuwa akizindua jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta barani Afrika (PAPU) lenye urefu wa ghorofa 17 sanjari na kuzindua Stampu na kuhudhuriwa na Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Posta kutoka kutoka katika nchi za Liberia, Afrika Kusini, Uganda, Malawi na Tanzania pamoja na wadau wa posta kutoka nje ya Bara la Afrika.

Alisema kuwa jengo hilo ni kitega Uchumi cha maendeleo ya Afrika litakuwa na ofisi zingine za kikanda,kimataifa na kumbi za mikutano na ni kichocheo cha maendeleo ya Afrika na kimeasisi maendeleo tuliyonayo .









Aidha alizitaka nchi wanachana ambazo zina malimbikizo ya ada kulipa sanjari na kuziomba ambazo hazijajiunga kujiungua na Umoja huo 

Alizipongeza nchi za Misri,Moroco, A lgeria,Zimbabwe ,Senegal na Nigeria kwa kutengeneza Stampu maalumu ambazo zitatumika kusafirishia barua duniani kote.

Alisema mradi huo umejengwa Kwa Ubia ambapo Tanzania kupitia mamlaka ya mawasiliano imechangia asilimia 40 na PAPU imechangia asilimia 60 na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa PAPU ili kufikia malengo na PAPU kiwe ni Kituo cha maendeleo barani Afrika .


Awali Waziri wa Habari,teknolijia ya habari na mawasiliano,Nape Nnauye,alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika ni kutimiza ndoto za Mwalimu Julius Nyerere ambae January 18 mwaka 1980 kwenye mkutano wa Umoja wa nchi huru za Afrika OAU uliofanyika Mjini Arusha,alioomba makao makuu ya Umoja huo yajengwe Arusha na Serikali imetimiza ndoto hiyo ya miaka 43 .


Alisema kuwa uzinduzi huo ulitanguliwa na kikao cha 43 cha Mawaziri wa masuala ya mawasiliano pamoja na  utawala ambacho dhana yake imejikita kuwezesha Sekta ya Uchumi na biashara ambapo Mawaziri wamekubaliana kuhamasisha Serikali zao kuwekeza vipaumbele kwenye Umoja huo na nchi yetu itanufaika na muingiliano wa wataalamu 


Alisema sasa ni wakati wa bara la Afrika kufanya  biashara kati ya nchi zetu  na hatuna sababu kuendelea kupelekwa utajiri wa Afrika nje ya Afrika tukishirikiana kupitia Umoja wa Posta  PAPU) tunaweza kuendeleza bara letu kiuchumi .


Jengo hilo la ghorofa 17 limejengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Nchini China,limegharimu shilingi bilioni 54.8 sawa na Dola milioni 21.89 ambapo Tanzania imechangia  asilimia 40 na PAPU asilimia 60.


Ujenzi ilitokana na kikao cha Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika,AU kilichofanyika Juni mwaka 2020  Mjini Abjan Nchini Ivory coast.


Mkuu wa shirika la Posta Nchini,Macrice Mbodo ,alisema kuwa posta haitakufa,kinachofanyika ni kufanya mageuzi ya kutosha kusaidia maendeleo ya nchi za afrika.


Alisema hii ni posta ya Kidigitali ambayo unaweza kununua chochote kupitia mtandaoni na simu ya kiganjani  na kufuatilia mzigo  na ukapata huduma bila kwenda ofosini.


Ends..

Post a Comment

0 Comments