Na Joseph Ngilisho Arusha
Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha ,kimemtaka mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo [CCM] kutengua haraka kauli yake iliyojaa dhihaka dhidi ya rais Samia Suluhu kwa viongozi anaowateua au atoke ndani ya ccm.
"Sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha tunakishauri chama chetu ni wakati mwafaka wa kuchukua hatua dhidi ya mbunge huyu na kama anaona anabanwa chama kimruhusu atoke"
Kauli hiyo ameitoa katibu wa umoja huo, Ibrahimu Kijanga wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.
Kijanga alisema kuwa Gambo amekosa nidhamu na kwa muda mrefu amekuwa kirusi ndani ya chama kutokana na kauli zake tata anazozitoa dhidi ya wateule wa rais akiwalenga viongozi wa mkoa wa Arusha .
Akizungumzia kauli ambayo Gambo ameitoa hivi karibuni katika mkutano wa wakuu wa shule za sekondari katika shule ya sekondari Arusha, Kijanga alisema Gambo amekosa nidhamu kwa kutoa maneno ambayo yamekifedhehesha chama hicho .
Maneno yanayodaiwa kusemwa na Gambo ni kwamba "Kazi ya mbunge ni kuwatumikia wananchi ila kazi ya wateule wa rais ni kumfurahisha aliyewateua ndugu zangu ukiangalia hayo maneno yamejaa dhihaka kwa rais".
"Pamoja na mambo mengine Gambo alizungumza maneno yaliyojaa dhihaka kwa mh Rais lakini pia kwa wateule wa rais katika mkoa wa Arusha ,Maneno yale kama umoja wa vijana yametufedhehesha ndio maana tukasema tuje kuongea na waandishi wa habari"
"Kama ataendelea na tabia hiyo tunafikiria kutoa mapendelezo kwa wakuu wa chana"
"Naamini Gambo alikuwa Dc na baadaye aliteuliw kuwa mkuu wa mkoa ina maana alikuja kuimba mapambio sisi tunaamini kwamba wateile wote walioletwa na mh Rais wanakuja kuwatumikia watanzania"
"Wateule wote wa mkoa wa Arusha walioletwa na mh Rais na mwenyekiti wa ccm wameletwa kuja kuwatumikia watanzania na wanafanyakazi nzuri kama zipo changamoto raia huwa anaziona"
"Sisi kama viongozi wa uvccm tunamkemea kwa ukali ache hizo tabia za kifedhuli tunamtaka ache hizo tabia za kejeli kwa wateule wa rais na ajifunze lugha za staha na ajifunze tamaduni za kuongea na kama hataki atoke ndani ya ccm"
"Hizi ni kauli za kejeli, kauli za dhihaka kauli za dharau aziache na kusema watanzania wanaminywa hawana uhuru serikali inatumia mabavu aziache serikali ya Rai Samia inafanya kazi nzuri sana"
"Sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha tunakishauri chama chetu ni wakati mwafaka wa kuchukua hatua dhidi ya mbunge huyu na kama anaona anabanwa chama kimruhusu atoke"
Ends...
0 Comments