Na Joseph Ngilisho,Arusha
Wadau wanaotoa huduma za bima Kanda ya Kaskazini wameiomba Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)kuboresha kasi ya mifumo ya kieletroniki ili kudhibiti mianya ya udanganyifu unaofanywa na watumiaji wa bima nchini.
Aidha TIRA imewataka watumiaji wa gereji kutumia fursa za bima ili kupata uhalisia wa malipo kutokana na kazi wanazofanya na kuepuka udanganyifu na kutoa agizo kwa mawakala wa bima nchini kujibu wateja malalamiko au hoja zao kwa maandishi kwamujibu wa kanuni na taratibu zinazotakiwa .
Wakitoa maombi yao katika mkutano wa Kupokea na Kusikiliza Maoni na Malalamiko ya Bima Kanda ya Kaskazini,baadhi ya wadau mbalimbali bima akiwemo Estomii Mlay aliomba
TIRA iboreshwe huduma zake za mifumo ya kieletroniki ili kurahisisha utoaji huduma bora kwa
"Kunaudanganyifu unafanywa na watoa huduma ikiwemo wanaokata bima mbalimbali za vyombo vya moto hivyo tunaomba mboreshe huduma za kieletroniki ili kudhibiti uongozo unaofanyika katika ulipaji wa bima kwenye vyombo mbalimbali vya moto na vingine"
Huku Ofisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Arusha,Joseph Michael aliomba TIRA kuboresha mifumo yake ili kudhibiti udanganyifu wa ukataji wa leseni za vyombo vya usafiri unaofanywa na baadhi ya mawakala wa bima nchini
Naye Saimon Mkoma kutoka Boma Ng'ombe wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ambaye aliunguliwa na nyumba yake mwaka jana ikiwemo gari na vitu vinginevyo vya thamani lakini licha ya kutoa vielelezo vyote hadi sasa hajalipwa fedha na badala yake kampuni bima ya Reliance Insurance imekuwa ikimzunguusha na familia yake ikikosa mahali pa kuishi na alikata bima kubwa ya nyumba na gari.
"Sielewei kwanini wananizunguusha kunilipa fidia yangu ilhali nilikata bima kubwa ya majanga na nimeunguliwa na vitu vyote sasa naomba msaada kamishna maana sipati majibu hata kwa maandishi"
Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Reliance Insurance ,Raphael Urassa alikiri faili la mteja wao linafanyiwa kazi na alisema shauri lipo kwa mchunguzi na linafanyiwa kazi na hivi karibuni atapewa mrejesho wake
Ambapo Kamishna Kamishna wa TIRA Nchini,Dk,Baghayo Saqware alisema inaonyesha kunaidhaifu wa kujibu wateja wa bima kwa maandishi na wahusika whawasimamii kanuni zinazopaswa kufanyika hivyo alitoa siku 14 kwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masuala ya Bima kushugulia suala hilo ili mafao ya bima yake ya kuunguliwa nyumba yake na vitu vyake ili aweze kulipwa .
Pia alitoa rai kwa wamiliki wa gereji kanda ya kaskazini kujiunga na TIRA ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani hivi sasa TIRA inaboresha mifumo yake ya kieletroniki kwani hivi wanataka kuona soko la bima linaenda kwa kasi na si kuwa ni soko la udanganyifu.
Mwisho
0 Comments