Picha kwa hisani ya mtandao hazihusiani na tukio hilo
Na Ngilisho TV , Ngorongoro
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wameshambuliwa kwa mikuki, mishale Ngorongoro nankundi la vijana zaidi ya 200 wa kimasai wilayani humo
Waandishi hao waliokuwa wakifuatilia uhamishwaji wa wananchi wa Ngorongoro kwenda maeneo mengine, walikutana na kundi la vijana waliobeba mikuki, mishale na mapanga waliowashambulia.
Zaidi ya vijana 200 wa jamii ya kimasai (morani) eneo la Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha wamewavamia na kuwajeruhi waandishi wa habari na mkalimani aliyeambatana nao.
Waandishi hao wamekuwa wilayani humo wakipata uelewa wa kwa nini Serikali inashauri wahame kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo kwenda Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Waandishi waliojeruhiwa ni pamoja na Ferdinand Shayo wa ITV, Denis Msacky (mwandishi wa kujitegemea), Habib Mchange (Jamvi la Habari), mkazi mwingine wa Ngorongoro, Lengai Ngoishie pamoja na mwandishi wa habari hizi.
Vijana hao walikuwa wamebeba mapanga, mikuki, sime na mishale.kati tukio hili linatokea Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Oleshangai, alikuwepo eneo la tukio na baada ya vijana hao kuvamia na kujeruji futwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala amesema anatuma askari kufika eneo hilo la tukio
0 Comments