Na Joseph Ngilisho Arusha
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameipongeza STAMICO na kubainisha kuwa katika miaka miwili iliyopita ilikuwa inafikiriwa kufutwa kutokana na utegemezi lakini sasa wameweza kuchangia hadi gawio kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
Akifungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma jijini Arusha, Rais Samia alisema kumekuwa na baadhi ya Wizara ambazo zimekuwa zikiomba michango kutoka katika taasisi zilizo chini ya Wizara zao kipindi zinapoishiwa bajeti ya matumizi mengineyo (OC).
“Wizara nyingi zimefanya mashirika kuwa vyanzo vya mapato. Mashirika yanapaswa kuchangia gawio … Wizara zinaweka mikono katika mapato ya mashirika hii haitakiwi kama tunataka mashirika yazalishe tusiyaingilie,” alisema Rais Samia jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Rais Samia kuna mashirika yaliundwa kujitegemea lakini yameshindwa kujitegemea na leo ni tegemezi serikalini na pia hayazalishi vizuri.
Rais Samia alisema Serikali imeshatoa pesa nyingi na sasa haiwezi kuendelea kutoa pesa kwa taasisi ambazo hazizalishi.
0 Comments