TCCIA YAWANOA MACHINGA,WALEMAVU NA VIJANA ,MEYA ARUSHA AWAAHIDI MIKOPO NAFUU

 

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA,kimetoa mafunzo ya uhusishwaji wa kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo(Machinga),Vijana, akinamama wa sokoni na watu wenye ulemavu. 

Akifungua mafunzo hayo Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maxmilliane Iranghe, amesema jiji la Arusha litatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu"Tumetenga takribani shilingi Billioni 4, Ela hii ikienda kwenye mzunguko itawatoa wafanyabiashara mahali walipo kwenda sehemu wanapotaka kuwa "alisema.

Pia aliwaasa makampuni mengi kuendelea kuandaa mafunzo kwa wajasiriamali kwa kuwapatia elimu itakayowainua kibiashara ilikuendelea kutengeneza wafanyabiashara wengi na wakubwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa TCCIA Arusha,Walter Maeda amesema kuwa wameaanda washa hiyo ilikuwapa motisha wafanyabiashara wadogo na wamachinga kuweza kufanya kazi kwa kujiamini na kufanyahiashara katika mazingira ya usafi.




Pia aliongeza kwa kusema kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kujijenga vizurii katika mazingira yake ya kazi na kuwa na vitambulisho maalum iliviweze kuwasaidia wao kutambuliwa na jiji la Arusha wakiwa kama wafanyabiashara iliwaweze kupata mikopo nafuu kwaajili yakuendeleza biasharaa zao.


Kwa upande wake Afisa biashara wa TCCIA, Charles Salvatory Makoi, alisema wameaanda mpango huo wa mafunzo kwa wakinamama wajasiriamali ilikuweza kujia ni namna gani wanaweza kuendesha biashara zao kwa kisasa zaidi

"Tuna mpango wakuwawezesha kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu na kuwakutanisha na wafanyabiashara mbalimbali "alisema.





Ends...


Post a Comment

0 Comments