TAZAMA WAZANZIBAR WALIVYOZAMA NDANI YA MGODI WA TANZANITE MERERANI,NAIBU SPIKA AMKUBALI MWEKEZAJI WA KAMPUNI YA FRANONE,"UWEKEZAJI WAKE UNATIJA KWA TAIFA'

Na Joseph Ngilisho MERERANI 

Naibu spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, ameridhishwa na uwekezaji wa madini ya Tanzanite  yanayochimbwa na wazawa katika mgodi wa Mererani na kutaka madini hayo yatangazwe zaidi ili kuwavutia wawekezaji na wanunuzi wakimataifa.


Akiongea mara baada ya kutembelea mgodi wa kitalu c iliopo Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, unaomilikiwa kwa ubia wa serikali pamoja na mchimbaji mzawa,Onesmo Mbise kupitia kampuni yake ya Franone Mining and Gem co.  Ltd.

Naibu spika huyo akiwa ameambatana na mawaziri na wajumbe wa baraza la wawakilishi na baadhi Yao kuzama NDANI ya mgodi huo.

Alimpongeza mwekezaji huyo na kudai kuwa uwekezaji wake unatija kwa taifa na unawanufaisha watanzania na kutokana na kuajiri watanzania wengi na kwamba ipo haja kwa wazawa kuwekeza zaidi katika Madini hayo na kuwataka wazanzibari kutafuta uwekezaji wa madini hayo.

"Sisi kama viongozi wa baraza la wawakilishi Zanzibar tumeridhishwa na uchimbaji wa madini ya Tanzanite, Mererani na tunakila sababu ya kuitangaza Mererani ndani na nje ya nchi na tumeona namna ambavyo watanzania wenzetu wanashiriki kukuza uchumi wa taifa letu kupitia sekta ya madini hayo"


Alisema baraza la wawakilishi litahakikisha rasilimali ya madini inatumika vizuri na watanzania wote wananufaika na madini hayo 

"Tumejipanga kwenda kuwashawishi wazanzibari kuja kuwekeza katika mgodi wa Mererani na hii inawezekana na tunahitaji wawekezaji wazawa zaidi wenye uchungu na nchi yao"


Naye Vitus Ndakize, mtaalamu wa Madini katika kampuni ya madini ya Franone ,alifurahishwa na ujio wa viongozi  hao kutoka zanzibara ambao walipata fursa ya kuzama mgodini na kujionea madini hayo yanavyojimbwa ardhini .

Aliwataka wawakilishi hao kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzanite duniani.

Alisema kuwa serikali iliwakabidhi mgodi huo Julai mwaka 2022 baada ya kusimama kwa miaka mitano na waliufanyia usafi na ukarabati na  Januari mwaka huu walianza uzalishaji na wamefanikiwa kuzalisha ajira kwa watanzania wapatao 330 huku ajira zisizorasimi ni zaidi ya 1000.





Ends.. 


Post a Comment

0 Comments