TANAPA NA KAMPUNI ZA UTALII KUADHIMISHA MIAKA 62 YA UHURU KIVINGINE , WATANZANIA KUPELEKWA KILELENI MLIMA KILIMANJARO 'LIVE'

 
Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na makampuni ya waongoza watalii nchini limepanga kuadhimisha miaka 62 ya uhuru kwa kuwapeleka idadi kubwa ya watanzania katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.


Hayo yameelezwa na naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA Herman Batiho wakati akiongea na vyombo vya Habari makao makuu ya TANAPA jijini Arusha,na kueleza namna watakavyo sherehekea miaka 62 ya uhuru yanayofanyika kila mwaka desemba 9,na kusema kuwa mwaka huu wamepanga kufanya tukio hilo la kihistoria kwa kuongeza idadi ya watanzania kupanda mlima Kilimanjaro.
"Maadhimisho haya yamekuwa yakifanyika kwa kupandisha bendera ya nchi yetu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Tukio hili limekuwa likihusisha kikundi cha wanajeshi wachache wakishirikiana na askari wa Hifadhi za Taifa Tanzania kwa uratibu wa kampuni ya utalii ya ZARA"lakini awamu hii tunatarajia kuwashirikisha zaidi watanzania.

Aidha, Kamishna Batiho aliongeza kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania limeongeza wigo kwa kushirikiana na mawakala wote wa utalii kuratibu kampeni za twenzetu kileleni kwa lengo la kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani wakati wa maadhimisho hayo ya Uhuru .

“Kati ya kampuni zote tulizozialika kushiriki katika uratibu wa maadhimisho haya ni kampuni tatu ndio zimejitokeza kushiriki kampeni hii katika msimu huu wa tatu. Kampuni hizo ni ZARA, African Zoom na African Scenic.” Alisema Kamishna Batiho.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro Angela Nyaki ametoa rai kwa watanzania wote kushiriki kuadhimisha sherehe hizo za uhuru katika kilele kirefu zaidi barani Afrika. 
Nyaki alisema kwamba zoezi Hilo limekuwa likifanyika kila mwaka ila mwaka huu wamepanua wigo kwa kuongeza Idadi ya wananchi kupanda mlima huo.

Alisema kuwa kauli mbiu ya Mwaka huu ni "kuhamasisha utunzaji wa mazingira ukanda wa pwani" hivyo tutumie fursa hii kuutunza mlima huu Kwa Faida ya wageni pia kutambua barafu inaendelea kuyeyuka.

Alisema kwamba Serikali na wadau wa Utalii ni muda muafaka Sasa kujitoa kuendelea kuhakikisha maeneo ya ukanda wa pwani tunatunza mazingira Ili yasaidie mlima Kilimanjaro kuweza kuvutia barafu kuendelea kuwepo na watalii wa kimataifa kuvutika kuja nchini kupanda mlima wetu.

Kwa Upande wake Meneja uhusiano wa kampuni ya Utalii ya ZARA Tours Ibrahimu Othman alisema kwamba wanaouzoefu mkubwa wa kuwapandisha Watanzania kuadhimisha miaka ya uhuru kama miaka iliyopita Kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ Pamoja na viongozi wa Tanapa.

Alisema ndio maana Kwa nafasi kubwa wamewashirikisha Watanzania na hii ni kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa nchi yetu kama ilivyo mwaka Jana tuliweza kupanda na mabalozi Taasisi na mashirika lakini tunaongeza wigo kuwakaribisha viongozi wote kuanzia Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Taasisi na Watanzania Kwa ujumla.

Awali Mkurugenzi wa kampuni ya African Slenic Safari Elisimbo Natai Amesema kwamba alisema kwamba njia ya Lemosho ni Moja ya njia nzuri zinazokuonyesha mlima wote hivyo ni fursa nzuri kwa Watanzania watakaojitokeza kufanya utalii wa Ndani kufika kujionea madhari nzuri ya mlima wetu.
 







Ends...

Post a Comment

0 Comments