Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC,dkt.Peter Mathuki amesema kuwa kiwango cha biashara katika soko la pamoja kimeongeza kwa asilimia 13.4 kutoka dola bilioni 74.1 mwaka 2022 ukilinganisha na dola bilioni 65 mwaka 2021.
Alisema ongezeko hilo la biashara kwa nchi za EAC ni sawa na asilimia 11.2 na kufanikiwa kuingiza kiasi cha faida sh,bilioni 10.9 mwaka 2022 kutoka bilioni 9.8 mwaka 2021.
Akizungumzia hali ya jumuiya ya Afrika mashariki katika kipindi cha mwaka 2023 ,Mathuki alisema kufanya biashara kwa pamoja kwa nchi za EAC, kumeongezeka katika miaka mitatu iliyopita kwa asilimia 13 na sasa imefikia asilimia 16 baada ya soko la DRC kuongezeka na kukua kwa idadi ya watu zaidi milioni 300 kwa nchi za EAC.
"Mwaka huu wa 2023 mwezi wa kwanza na wa pili kiwango cha biashara kilifanyika katika nchi zetu kwa asilimia 16 na19 mwezi wa pili na tunatarajia kufikisha asilimia 20 na ndio tuliahidi na tunapongeza kwa nchi zetu za EAC na washkadau wetu "
Alisema manufaa hayo yametokana na kupanuka kwa soko la pamoja hasa mara baada ya nchi ya DRC kujiunga yenye watu takribani 100 na hivyo soko hilo la pamoja kupanuka na kufikisha watu zaidi 300.
Alisema sababu nyingine ni kuondolewa kwa changamoto ya vikwazo vya kibiashara lilivyokuwa vikilalamikiwa na wananchi katika mipaka yetu pamoja biashara ya sekta binafsi.
Alisema katika miaka miwili iliyopita vikwanzo 177 kati 184 viliondolewa na kubaki 7, ingawa kuna vikwazo vingine vimekuwa vikiongezeka.
Hata hivyo Dtk.Mathuki alibainisha kuwa sekretarieti wamelishauri baraza la mawaziri la jumuiya hiyo kuharakisha mchakato wa sarafu moja ufanyike kabla ya mwaka 2030 waliopanga.
"Mchakato wa sarafu moja kwa maoni yetu kama sekretarieti tunaona ufanyike kabla ya miaka 3 tunawasihi mawaziri wa fedha wapambane tuweze kupata sarafu moja tuweze kuwasaidia wananchi wetu na pia wawekezaji wakati tukisubiri mtangamano wa kisiasa kukamilika"
Alitoa mfano wa Jumuiya ya umoja wa ulaya AU wameanza na fedha yao Euro huku nchi zao zikiendelea na fedha zao za ndani jambo ambalo hata jumuiya yetu iaweza kufanya halafu fedha za ndani zikaondoka kidogo kidogo wakati huu tukiendelea na mchakato wa katibu ya mtangamano wa kisiasa.
Kwa mujibu wa Dtk.Mathuki alibainisha suala la mtangamano wa kisiasa kuwa wameanza na katiba za nchi wanachama na kwa nchi za Uganda South Sudan na Kenya na watafuatia nchi zilizobakia huku wakitarajia mchakato wa katiba kuanza mwezi wa sita mwakani wamekamilisha mchakato huo.
Ends..
0 Comments