Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala, katiba na sheria ,imeanza mchakato wa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ili kuipa nguvu ya kisheria tume ya Nguvu za Atomic Tanzani(TAEC)na kuahidi kulishauri bunge kupitisha sheria hiyo baada ya kujionea uwezo mkubwa wa Tume.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea makao makuu ya tume hiyo yaliyopo njiro jijini Arusha ,makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ,Florient Kyombo alisema ziara hiyo imelenga utekelezaji wa maadhimio ya bunge katika kuchakata mswada wa mabadiliko ya sheria sita ikiwemo inayoigusa tume hiyo.
"Tar 28 juni mwaka huu,tulipokea mswada ambao ulisomwa bungeni kwa mara ya kwanza na mswada huo ni washeria mbalimbali wa mwaka 2023 ambapo miongoni mwa sheria sita ambazo zinarekebishwa katika mswada huo ni sheria inayoiguza Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzani "
'Sisi kama wajumbe tulielekezwa na spika kushughulikia mchakato wa mswada huo na ilionekana ni vema tukaja kupata uelewa zaidi baada ya kupata mafunzo ya ndani na tumejidhatiti katika kushauri mswada huo"
Aidha Kyando aliipongeza TAEC kwa usimamizi na uratibu mzuri wa vifaa vinavyotumia mionzi hapa nchini na kuahidi kuishauri serikali iwekeze zaidi katika tume hiyo ilibkuhakikisha afya za watanzania zinakuwa salama zaidi.
"Tumepitia maombi ya mabadiliko ya sheria ambayo TAEC wanaona kwa kipindi hiki ni matamanio yao kwamba sheria ikirekebishwa inaweza kuwasaidia kufanya kazi zao vizuri tofauti na mwanzo qmbapo ilikuwa ukighundulika unaingiza mionzi kinyume cha sheria unafungiwa pekee "
Alisema mabadiliko ya sheria yanaenda kumpa nguvu mkurugenzi wa TAEC kukamata na kupiga faini kwa watu wanaoingiza mionzi bila kufuata utaratibu .
Katika hatua nyingine aliwatoa hofu wananchi juu ya uwepo wa athari za mionzi kwenye minara ya simu iliyopo karibu na makazi ya watu pamoja na mashine za ukaguzi (scanner) kwa kudai kuwa elimu walioipata katika tume hiyo imewafungua kuwa hakuna madhara yoyote kwa binadamu.
Awali mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Prof.Lazaro Busagala alisemabziara ya kamati hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao kutokana na elimu ya kuwajengea uwezo wa vitendo katika eneo la ulinzi wa mionzi na matumizi salama ya Teknolojia ya nyukilia na hivyo kendal kulishauri bunge vizuri ili watanzia wanufaike na Teknolojia ya nyukilia na kubaki salama.
Alisema changamoto kubwa kwa TAEC ni kukosa nguvu ya kisheria kuwashughulikia baadhi ya watu wanaowasimamia ambao wanaenda kinyume na tarabitu ikiwemo kushindwa kuomba leseni kwa wakati.
"Kama bunge litaridhia maombi ya mabadiliko ya sheria basi tunauhakika changamoto hiyo itakuwa imeisha"
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo,Edward Lekaita(Mb. Kiteto) alisema ziara yao katika kituo hicho ni kujionea utendaji kazi wa tume ili kuridhia mabadiliko ya sheria yaliyoombwa na TAEC.
"Nia yetu kuja hapa ni kuona na kulinganisha yale ambayo TAEC wanataka bunge litunge sheria ,kamati imejiomea na kujua baadhi ya vitu ,tumebaini hii ni taasisi muhimu sana inayoshughulikia masuala nyeti ya afya za watu na sisi kama wajumbe tutaenda kulishauri bunge"alisema Lekaita.
Naye mbunge wa Busanda ,Tumaini Magesa,alisema elimu walioipata TAEC ni vizuri ikatolewa pia kwa wananchi ili kuwasadia uelewa juu ya athari za mionzi kwenye chakula na manufaa yake.
"Sisi kama wabunge hatuwezi kupitisha sheria bila kujiridhisha ,hivyo uwepo wetu hapa umetusaidia kuielewa TAEC na shughuli zake, tumetembelea takribani maabara 12 na tumeona uwezo wa tume na tutaenda KULISHAURI bunge"
Ends..
0 Comments