SHAHIDI WA 18 KESI YA MAUAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA ,ADAI MSHITAKIWA (MIRIAM) ALIMSHIKIA BASTOLA

BY NGILISHO TV  

SHAHIDI wa 18 katika kesi ya Mauaji inayowakabili aliyekuwa mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake ameieleza mahakama kuwa aliyemtambua mshtakiwa wakati wa gwaride la utambuzi akisikia akisema kuwa Miriam alimshikia  bastola.


Shahidi Sophia Amir Shemzigo(46) na mama ntilie ambaye kwa sasa anaishi Songea, ameeleza hayo leo Agosti 21,2023 wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Edwin Kakolaki wa mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.


Washtakiwa katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 ni wifi wa marehemu, Aneth, mjane wa Bilionea Msuya; Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella.


Aneth alifariki dunia Kwa kuchinjwa shingoni Mei 25, 2016, usiku nyumbani kwake, Kibada Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo).


Akiongozwa na wakili wa serikali Generosa Montana,  Sophia ambaye zamani alikuwa akishi Dar es Salaam eneo la kurasini amedai kuwa, Agosti 7, 2023 akitokea kudai madeni yake ya chakula eneo la Jkt Mgulani aliitwa na askari polisi wa kituo cha Kilwa road akimtaka ashiriki Gwaride la utambuzi.


Amedai alikubali ndipo askari huyo atamchukua hadi nyuma ya kituo hicho cha polisi ambapo alikutwa wanawake wengine saba na yeye akawa wa nane.


"Tulipangwa mstari na msimamizi wa gwaride ambaye alikuwa ni askari wa kiume akatuambia kuna utambulisho na kwamba kuna mtuhumiwa wa mauaji anatakiwa kutambuliwa. Ndipo wakati wamesimama pale mtuhumiwa alipelekwa n kusimama pembeni yake.

Amedai kuwa baada ya kuwa wamejipanga mstari askari mmoja wa kike alimpeleka msichana  na kumwambia apite kwenye gwaride lile kwa nyuma na mbele


"Wakati anapita alipofika kwa mbele alimshika bega la kushoto mtuhumiwa akatamka 'Huyu ndio ambae alikuja nyumbani kwa tajiri yangu Kigamboni akanitishia kwa bastola na kuniambia ondoka'


Amedai baada ya hapo mtuhumiwa alichukiliwa na askari wa kike akaondoka nae na sisi tukapewa karatasi tukasaini na kuruhusiwa kuondoka.

baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, wakili wa utetezi Peter Kibatala alimuhoji mshtakiwa ambapo mahojiano yao yalikuwa:


Kibatala: Shahidi wakati unaongozwa na wakili hapo kutoa ushahidi, ulimwambia Jaji kwamba kwenye hii karatasi kuna namba zako za simu walizotumia kukuita?


Shahidi: Ndio


Kibatala: Ulimwambia Jaji kuwa yule mama aliyetambuliwa alikuwa hana alama yoyote, hajavimba au kuchubuka usoni?


Shahidi: Sikumwambia


Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe huna uhusiano wowote na afisa wa Polisi?


Shahidi: Sikumwambia


Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe hauna huba husuda na wala chuki na huyu dada?


Shahidi: Sijamwambia



Kibatala: Ulimwambia Jaji kwamba wewe ulikuwa huna wala humfahamu huyu mshtakiwa wala ndugu wa marehemu?


Shahidi: Sijamwambia




Kibatala:  Shahidi, hii kesi umekuwa reported kwenye vyombo vya habari je ulimwambiaJaji kwamba utambuzi wangu hauhusiani na kuona picha yake kwenye magazeti?


Shahidi: Sikumwambia


Kibatala: Shahidi ulimwambia Jaji wale maafisa wa Ukaguzi walimpa nafasi mtuhumiwa kumkataa yeyote pale?


Shahidi: Sikumwambia


Kibatala:  Shahidi umesema tu binti aliyekuja alisema maneno...


Shahidi: Ehee


Kibatala: Mwambie Jaji kama ulimsikia.aiitaja tarehe na mwaka


Shahidi: Hakutaja tarehe


Kibatala: Ulimsikia huyo dada akisema hata hivyo namfahamu niliwahi kumuona Mererani kwa mama Aneth 


Shahidi: sijamsikia


Kesi hiyo inaendelea kesho kwa shahidi wa 19 wa upande wa Jamuhuri kutoa ushahidi wake.

Post a Comment

0 Comments