SAKATA LA MFANYABIASHARA MONABAN KUPORWA KIWANDA KIBABE LAIBUKA UPYA MTOTO AWASHA MOTO, WAZIRI MKUU ATAJWA, WAZIRI KIJAJI AMPIGA STOP MBUNGE GAMBO

 Na Joseph Ngilisho , Arusha

Waziri wa Viwanda na Biashara ,Dk,Ashatu Kijaji ameahidi kushughulikia sakata la mfanyabiashara Dkt, Philemon Mollel la kunyang'anywa kimabavu kiwanda cha usagaji nafaka cha Monaban Trading & Farming Ltd kilicho Jijini Arusha.


Dkt,Kijaji aliyasema hayo Jijini Arusha wakati akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali kwaajili ya kubaini changamoto zao ili serikali kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji kazi.

Alisema amechukua hoja zilizotolewa na mtoto wa mfanyabiashara huyo Nathani Mollel na kwakua malalamiko hayo ya kunyang'anywa kiwanda yalimfikia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa basi ataenda kufuatilia na kujua ilikuwaje kisha kurudisha mrejesho kwa mhusika ambaye ni Mkurugenzi Monaban

"Nimesikia jambo hili lakini kwakua mmemtaja bosi wangu Waziri Mkuu,Majaliwa kuwa alikuwa anashughulikia sakata hili nitapata jibu kujua ilikuwaje kuwaje na kama Monaban alifanya makosa ataelezwa kama hajafanya tutasema hatua gani zichukuliwe katika jambo hili ila kwa sasa sitatoa jibu la moja kwa moja juu ya sakata hili"

Awali mtoto wa aliyekuwa Mwekezaji wa kampuni ya Usagaji nafaka ya Monaban Trading& Farming Ltd ,,Nathan Mollel alimuomba Waziri  Dkt, Kijaji kuwasaidia ili mali za baba yake ,Dkt, Philemon Mollel alizowekeza kwenye  kiwanda hicho zaidi ya sh, bilioni 20 zirudi baada ya  kunyang'anywa kiwanda hicho kimabavu ilhali mkataba wa uwekezaji wakiwanda hicho ukiwa haujaisha

Nathani alitoa  ombi hilo jana Jijini Arusha katika kikao cha wafanyabiashara juu ya kujadili changamoto zinazowakabili kilichoitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk,Kijaji sanjari na wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali, na kusema kilichofanyika kuwaondoa katika kiwanda hicho ni mabavu ambayo yameacha pigo sababu baadhi ya fedha walizokuwa wakiendesha kiwanda hicho walikopa benki na hivi sasa  benki inataka kutaifisha mali zilizopo kiwandani hapo ambazo zilichukuliwa

Alisema Mollel aliwekeza  katika kinu cha usagishaji cha NMC kilichochini ya bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (COPB) cha Jijini Arusha lakini licha ya juhudi za kumwona Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na maagizo yaliyotolewa kuhusu kiwanda hicho ili kumsaidia aweze kuendelea na uwekezaji katika a kupokonywa kimabavu wakati mkataba wake wa upangaji ukiwa bado unaendelea.


Alidai  kulikuwa na mazungumzo yanaendelea na waziri Mkuu Kasimu Majaliwa juu ya upangaji wake lakini ameshangaa kuondolewa kimabavu bila kufuata utaratibu.


Alisema  uwekezaji wake katika kiwanda hicho unafikia kiasi cha sh,bilioni 20 fedha ambazo zimetokana na mkopo kutoka mabenki mbalimbali hapa nchini baada ya kujidhamini na mali zake ikiwemo nyumba yake .


Alimuomba Dkt,Kijaji kuingilia kati suala hilo ili kubaini ukweli maana wamehangaika safari za Dodoma kumwona Waziri Mkuu ,Majaliwa naye alisema anashughulikia lakini hadi leo hawajapewa kiwanda chao na  wala kukaa meza moja na watu wa serikali kujua hatma yao kwani baba yao Monaban  alikopa mikopo benki kwaajili ya kuendesha kiwanda kile sasa wameondolewa kwa mabavu .

"Sasa kama mwekezaji mzawa amefanyiwa hivi hao wengine itakuwaje na sasa hivi baba yangu amekuwa askofu kaona bora amrudie mungu maana tulichofanyiwa hakikustahiki kama tulifanya makosa kwanini wasituambie kuliko kututoa kimabavu na mkataba wetu haukuisha tunaomba kujua hatma yetu"

Aliongeza kuwa wakati Mollel anawekeza katika kiwanda hicho mwaka 2007 alikuta kiwanda hicho kimekufa na kuamua kujenge miundo mbinu ikiwemo kununua mashine mpya za usagaji ,kuzungushia ukuta kiwanda hicho pamoja na kuweka vitofari kwenye sakafu ili kuondoa vumbi.


Alisema kuondolewa katika uwekezaji huo kumesababisha wafanyakazi zaidi ya 80 waliokuwa wameajiriwa kukosa kazi, huku Mollel akihofia kuvunja uaminifu wake na mabenki aliyokuwa akikopa fedha kwa ajili ya uwekezaji huo.


Akisimulia hali ilivyokuwa siku wakiondolewa kiwandani hapo miaka miwili  iliyopita alisema walivamiwa na askari polisi zaidi ya 10 wakiwa wameambatana na maofisa wa bodi ya nafaka na mpaka leo hawajui Mali za kiwanda zimekufa au la huku benki zikiwa zinataka kutaifisha mitambo iliyokuwepo kiwandani hapo.

Hata hivyo wakati Nathan  akimweleza Waziri huyo, mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo aliyekuwa Amelia meza kuu na waziri,aliingilia hoja hiyo alidai jambo hilo lipo kwa Waziri mkuu, lakini Dkt Kijaji alimjibu kuwa wachaa aendelee kueleza na mimi nipate kulielewa vema jambo hilo na kulipatia ufunbuzi. 

Ends.. 

Post a Comment

0 Comments