RAIS SAMIA KUTUA TENA ARUSHA,KUFUNGUA KIKAO KAZI AICC,MASHIRIKA 248 KUSHIRIKI

 Na Joseph Ngilisho Arusha 


RAIS Samia Suluhu anatarajiwa kufungua kikao kazi cha kwanza kufanyika cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali,utakaofanyika katika Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha huku mashirika zaidi ya 245 yakithibitisha kushiriki.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akitoa taarifa ya maandalizi ya kikao hicho na kusema mbali na Rais,Viongozi wengine watakaokuwepo ni pamoja na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge,Dkt Tulia Acksoni na mawaziri .

Alisema Augosti 21, Rais Samia,atakuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthelu Nchini,KKKT yatakayofanyika kwenye Chuo cha Makumura,kilichopo Makumura  Wilayani Arumeru.

Mwenyekiti wa Jukwaa la mashirika ya umma  na Taasisiza Serikali ,Sabasaba Moshingi,alisema kuwa hicho ni kikao kazi cha kwanza kufanyika lengo la kikao hicho ni kuziwezesha Taasisi na mashirika kutengeneza faida na kutoa huduma bora na nzuri.

Alisema kuwa Jumla ya taasisi 248 yakiwemo mashirika ya umma na Taasisi za Serikali yatashiriki kikao hicho ambapo wajumbe zaidi ya 1000 watakuwepo .

Alisema kuwa kauli mbiu ya kikao hicho ni mwelekeo mpya wa usimizi na uendeshaji wa Taasisi za umma.

Awali Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano ya kimataifa,AICC,Balozi mstaafu Ephraimu Mafuru,alisema nchi yetu imefikia ya nafasi ya  tano barani Afrika Kwa kuandaa mikutano ya Utalii kimataifa .

Alisema nchi ambazo zimetutangulia ni Afrika kusini,Moroco,Rwanda,na Misri,na bado nchi yetu inaendelea kufanya vizuri kwenye Uchumi wa mikutano ya kimataifa na Katika kipindi cha miaka mitano ijayo tunaweza kufikia nafasi ya tatu bora.

Alisema kuwa nchi yetu ni mwanachama wa Taasisi ya ICA,ambayo ni Taasisi inayoandaa mikutano mikubwa inayofanyika barani Afrika,na Kila mwaka AICC,inapokea taarifa kutoka kwenye Taasisi hiyo imefikia nafasi ya ngapi Katika kuandaa mikutano ya Uchumi wa utalii.

Alisema mwaka 2019  Katika mikutano iliyofanyika barani Afrika nchi yetu iliweza kuandaa mikutano 19 ambayo ni sawa na asilimia 30% ya mikutano yote inayoaandaliwa na Taasisi hiyo.

Aliongeza kuwa mwaka 2022 nchi yetu ilifanikiwa kuandaa mikutano 18 iliyofanyika barani Afrika na mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia,ya kufungua nchi na tupo kwenye Uchumi wa mikutano.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Viongozi mashirika ya umma na Taasisi za Serikali ,Latifa Mohamed Hamisi,amesema kuwa wanatarajia kupata mwelekeo mpya wa usimamizi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali Katika kutoa huduma bora na baada ya kikao hicho kutakuwepo na mabadiliko makubwa ya utendaji ma usimamizi wa mashirika hayo na Taasisi za Serikali.

Ends..

Post a Comment

0 Comments