RAIS SAMIA AMWAGA BIL.37 ATC ARUSHA, KUFUFUA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA MJERUMANI,KIKULETWA,DC ASEMA RAIS SAMIA AMEHESHIMISHA

Na Joseph Ngilisho, HAI

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha sh, bilion 37 kwa ajili ya kufufua kituo cha umahiri katika ufundishaji na utafiti wa teknolojia za nishati jadidifu cha Kikuletwa kilichoanzishwa na wajerumani  mwaka 1930 na kufa miaka  30 iliyopita  kilichopo kijiji cha Chemka Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro. 


Aidha fedha hizo zitatumika pia katika ujenzi  wa kituo cha  kuzalisha mafundi umeme na mitambo kitakachochukua wanafunzi wapatao 600 watakaotekeleza Miradi ya kimkakati ikiwemo bwawa la Mwalimu Nyerere JNHPP na Shirika la Umeme Tanesco.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Amiri Mkalipa Wakati alipotembelea miradi mbalimbali ikiwemo kituo hicho cha kuzalisha umeme inayotekelezwa na Chuo cha Ufundi Arusha ATC ambao ukikamilika utazalisha megawati 1.65 na kuhudumia pia wananchi wa kijiji cha Chemka kilichopo eneo hilo.

"Rais Samia amekipa heshima kubwa chuo hiki cha ufundi Arusha kwa kukipatia sh,bilioni 37, lindeni heshima ya mama kwa kuzitumia vema fedha hizo "

Alisema kwamba Mradi huo utakapokamilika utasaidia chuo kuuza umeme na wananchi wanaozunguka kunufaika na huduma hiyo jambo ambalo kituohicho kitazalisha wataalamu ambao watasaidia katika miradi mbalimbaliitakayotekelezwa na serikali hapa nchini.

"Katika utekelezaji wa mradi huu lazima mhakikishe uzalendo unawekwambele sanjari na matumizi sahihi ya fedha bila kusahau kumaliza ujenzindani ya muda uliopangwa  ili manufaa ya Kituo hicho yaweza kuwanufaisha kizazi kijacho tofauti na awali ulipotekelezwa"

Awali akitoa Taarifa ya Mradi huo Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha ATC Dkt.Mussa Chacha  alisema kuwa mradi huo wa kituo cha umahiri kutazalisha Wataalamu wa nishati jadidifu watakaokuwa na uwezo wa kufanyakazi na kuzisaidia nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na duniani kote kwenye miradi mikubwa ya umeme ya kimkakati.

Alisema kwamba mradi huo unatarajiwa kumalizika ifikapo oktoba mwaka 2024 huku akimtaka mkandarasi kuendeleza kazi kwa kasi ili kuweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa sanjari na kuhakikisha wanailipa halmashauri mapato yake.


"Tumejipanga kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa sanjari na maagizo ya Mkuu wa wilaya ya hai yanatekelezwa kwa haraka ili kuondoa changamoto za mapato ya halmashauri ambayo mkandarasi hajalipa tokea kuanza ujenzi wa chuo"

Naye Mkuu wa kituo cha mafunzo cha Kikuletwa, Sithole Mwakatoge  alisema kuwa kwa sasa kuna jumla ya wanafunzi wapatao 55 wanaochukua mafunzo ngazi ya cheti ya fundi Umeme,ujenzi ,Fundi Bomba,Fundi Mitambo ya umeme wa maji na umeme wa jua.

Alisema kabla ya kufa kwa mtambo huo mwaka 1998 ulllikuwa unazalisha megawatt 1.2  na wamejipanga kuzalisha megawati 2.65.

Kwa Upande wake Mjukuu wa Mmoja ya waanzilishi wa Kituo hicho  chakuzalisha Umeme Kikuletwa aliyefika kutembelea kituo hicho kilichokufa miaka 30 iliyopita , WOLF LEACK kutoka ujerumani alisema kwamba Babu yake alikuwa mkandarasi alietekeleza mradi huo wa kituo cha kuzalisha umeme ambapo baba yake alizaliwa hapa nchini mkoani Kilimanjaro wilaya ya Moshi mwaka 1936 wakati wa Ujenzi wa kituo.








Ends.




Post a Comment

0 Comments