POLISI YAMWACHIA USIKU MBUNGE ALIYEKAMATWA,KWA KUPIGA WAANDISHI,ADAI ALIGOMABKULA SIKU TATU

Na Joseph  Ngilisho Arusha 

Jeshi la Polisi  Mkoani hapa limemwachia huru kwa dhamana Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai ambaye alikuwa anashikiliwa akituhumiwa kuratibu kundi la Morani kushambulia wanahabari wakati wakitekeleza majukumu yao wilayani humo.



Akizungumza baada ya kuachiwa Ole Shangai amesema kwa siku tatu tangu alipokamatwa aligoma kula na baada ya kujisalimisha Karatu alisafirishwa saa saba usiku Agosti 22 kurudishwa Arusha na alikuwa Kituo cha Diplomasia jijini Arusha.

Mbunge huyo alijisalimisha polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa kuhusika na tukio la kuratibu kundi na kushambuliwa waandishi wa habari lililotokea Agosti 15, 2023.



Post a Comment

0 Comments