MTAKWIMU MKUU :IDADI YA WATALII YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 57.7,SERIKALI YATENGENEZA DOLA MIL 2.5


 Na Joseph Ngilisho, Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu na Uchumi Nchini,Daniel Masolwa amesema katika kipindi cha mwaka jana idadi ya Watalii  iliongezeka na kufikia watalii  milioni 1.4 ikilinganishwa na watalii 922,692 mwaka 2021 na hiyo ni sawa na  ongezeko la asilimia 57.7


Masolwa ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha na kusema kuwa kiasi hicho cha Watalii serikali ilifanikiwa kuingiza dola za Kimarekani zaidi ya milioni 2.5 ikilinganishwa na dola za Kimarekani zaidi ya milioni 1.3 zilizoingizwa mwaka 2021.

Alisema kuwa wastani matumizi ya Mtalii mmoja kwa siku walioingia mwaka jana iliongezeka hadi dola za Marekani 214 ikilinganishwa na dola za Kimarekani 199 mwaka 2021 na hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 92.9


Alisema Nchi ya Marekani iliongoza mwaka jana kuingiza watalii Nchini kwa kuingiza watalii 100,600} kuja kuangalia vivutio ikifuatiwa na Nchini ya Ufaransa watalii 100,371} ,Ujermani watalii 67,718},Uingereza watalii 60,116} na Poland watalii 46,431}.


Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa katika Watalii waliokuja kutalii mwaka jana kutoka Bara la Afrika ni pamoja na Nchi ya Kenya watalii 166,324,Burundi watalii 100,851 ,Zambia watalii 46,787,Malawi watalii 44,438 na Rwanda watalii 44,288.


Masolwa alisema pia katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu idadi ya watalii imezidi kuongezeka zaidi na katika kipindi hicho watalii imeongezeka tofauti na mwaka jana kwani watalii 759,327 waliingia katika kipindi hicho ikilinganishwa na mwaka jana watalii 575,397 waliingia katika muda huo mwaka jana na hiyo ni ongezeko la asilimia 31.9



Alisema watalii wengi walioingia nchini katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu ni kutoka katika nje ya Bara la Afrika na kipindi hichi Nchi ya Marekani iliendelea kuongoza kwani iliingia watalii 51,674,Ufarasa watalii 48,696} ,Ujermani watalii 39,789 ,Uingereza watalii 29,770 na Nchi ya Italia iliingiza watalii 29,554.


Aidha watalii walioingia nchini katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu kutoka nchi za Bara la Afrika walitoka katika nchi za Kenya watalii 93,488,Burundi watalii 47,418 ,Rwanda watalii 26,899,Zambia watalii 25,372 na Nchi ya Uganda watalii 20,727 walikuja Nchini kutalii katika vivutio mbalimbali vilivyoko katika hifadhi zetu.


Mkurugenzi Masolwa alisema kuwa watalii wengi waliokuja nchi kutalii katika vivutio vyetu mwaka jana na mwaka huu tafiti za ofisi yake zinasema kua walipata taarifa kupitia uhamashishaji wa serikali uliofanywa na kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na filamu ya ya Tanzania The Royal Tour,ofisi za Ubalozi,ndugu na jamaa na watoa huduma kwa watalii {Tour Operators} .


Alisema Serikali itaendelea kutangaza zaidi vivutio vya utalii nje ya nchi kwa kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania na watalii wengi walifika nchini kwa lengo la kupumzika na idadi kubwa ya watalii waokuja nchini kutalii ni utalii wa wanyamapori na utalii wa ufukweni.


Mwisho


Post a Comment

0 Comments