MGOMO WA DALADALA NA BAJAJ ARUSHA WAMNG'OA MWAKALEBELA WA LATRA ARUSHA,OFISA MPYA ATINGA OFISINI NA MKWARA WA KUFUTA LESENI DALADALA ZILIZOGOMA

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Migomo ya daladala na bajaj inayoendelea bila kupatiwa ufumbuzi katika jiji la Arusha,imetajwa kumg'oa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini (LATRA) mkoa wa Arusha Amani Mwakalebela baada ya kushindwa kutatua migogoro hiyo na kusababisha usumbufu kwa wananchi ,wafanyabiashara na wanafunzi kukosa usafiri.

Mwakalebela amepata uhamisho wa  ghafla wakati bado sakata la mgomo wa daladala halijapoa huku mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa ameunda kamati ya usuluhishi juu ya mgogoro  huo na kuja na majibu.

Leo jumatatu wakati ofisa mpya Mwandamizi wa LATRA Joseph Maico akitinga ofisini rasimi kuchukua nafasi ya Mwakalebela, daladala zimegoma tena na kusababisha adha kwa wananchi.
Afisa Mpya wa LATRA Mkoa wa Arusha, Joseph Maico 

Akiongea  na vyombo vya habari ,Maico aliwataka wamiliki wa daladala katika jiji la Arusha, kusitisha mgomo wao mara moja na kurejesha usafirishaji kwa kuwa mamlaka hiyo imeanza kutekeleza maoni ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa .

Alisema iwapo daladala zitaendelea na msimamo wakutotii mamlaka ya kuwataka wasitishe mgono mara moja,LATRA itafuta leseni zao mara moja kama sheria inavyotaka.

"Mimi nimeingia ofisini Leo  jumatatu Agost 14,jana tulikutana na viongozi wa vyombo vya usafirishaji kwa lengo la kutambulishana kama afisa mpya wa LATRA Arusha, na Leo nimejaribu kuzungukia baadhi ya maeneo ikiwemo ruti za daladala zaidi ya 145 ,mimi na wenzangu tupo katika hatua ya kutekeleza maoni ya kamati hiyo "

Kuhusu ofisa aliyekuwepo kuondolewa  ghafla katika kituo chake cha kazi mkoani Arusha, alisema ni uhamisho wa kawaida haihusiani na mgogoro wa daladala na bajaj. 

Mgomo wa daladala umerudia tena leo jijini hapa, huku madereva wa magari hayo wakimwomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati mgogoro uliopo kati yao na madereva wa pikipiki za matairi matatu maarufu kwa jina la Bajaj.

Mgomo huo unafanyika leo Agost 14 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo, ukiwemo mgomo uliofanyika Julai Mosi na mwingine ukafuatia wa Julai 3 mwaka huu, ambapo madereva daladala wamekuwa wakishinikiza kuondolewa kwa usafiri wa bajaji katika barabara wanazohudumu kwani zinawanyima biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, mmoja wa madereva daladala Herman Elias alisema katika mgomo wao wa pili, Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela aliitisha kikao cha madereva hao na kusikiliza madai ya daladala na Bajaji na kuahidi kuchukua hatua ya utatuzi.



Adha ya usafiri inavyoathiri mpaka makondakta na madereva ,kondakta akionekana kuuchapa usingizi bila mlo wa mchana
Ends..











Post a Comment

0 Comments