Na Joseph Ngilisho Arusha
UJENZI wa Kituo kikuu cha mabasi katika Jiji la Arusha,kinachojengwa eneo la Bondeni seed,unatarajia kuanza mapema September mwaka hu baada ya kumalizika Kwa mgogoro uliokuwepo kati ya halmashauri hiyo na mmiliki wa eneo hilo na tayari Mzabuni ameshapatikana.
Meya wa halmashauri ya Jiji la Arusha,Maximilian Illanghe,ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokuwa akizingumza na Vyombo vya habari akitoa ufafanuzi wa maamuzi ya kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika jana Augosti 24.
Alisema Ujenzi huo umechelewa kutokana na changamoto iliyokuwepo na hivyo kuilazimu halmashauri kukaa na mmiliki wa eneo hilo na hivyo Ujenzi utaanza.
Meya ,alisema kuwa halmashauri hiyo ina vipaumbele vyake ambavyo vitatekelezwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2023/2024.
Alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuongeza makusanyo ya mapato, kujenga barabara zote za ndani ili zipitike,kujenga Vivuko, kuweka taa za barabarani ,kujenga Vyumba vya madarasa na kukarabati matundu ya vyoo vya shule,kutoa fedha Kwa Tarura kwa ajili ya ujenzi barabara mbalimbali na kukamilisha miradi yote,kujenga Vituo vya afya .
Alisema kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani yanayofikia sh, bilioni 48 ,halmashauri hiyo inatarajia kujenga Ukumbi wa kisasa wa mikutano Katika kata ya Levolosi ikiwa ni chanzo cha mapato.
Meya,alisema mwaka huu pia halmashauri imepanga kujenga masoko mbalimbali ikiwemo la Samunge ambalo litakuwa la ghorofa mbili,Soko la Kilombero, soko la kisasa Engutoto ambapo wametenga eneo la hekari 8 .
Alisema halmashauri itaendelea na kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya inayojengwa Engutoto ,baada ya kuvunja mkataba wa Ujenzi na Mkandaradi wa awali na kupata Mkandaradi mpya na hadi Desemba mwaka huu hospitali hiyo itakuwa imekamilika .
Alisema halmashauri hiyo imetoa eneo kwa Shirikishi la mpira wa miguu Nchini,TFF,eneo la kujengwa Kituo cha mafuunzo ya michezo ,pia imetoa eneo lingine Kwa Serikali Kwa ajili ya kujenga Uwanja mpya wa kisasa wa mpira wa miguu kata ya Olmot,kwa ajili ya michezo ya Afrika..
Kuhusu fedha za mikopo iliyotolewa Kwa Vikundi mbalimbali inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya Meya ,amesema halmashauri inatarajia kununua magari Kwa ajili ya kurahisisha Ufuatiliaji wa mikopo hiyo ambayo haijarejeshwa na imekuwa ni changamoto.
Meya alisema halmashauri hiyo haitamfumbia macho mtu yoyote ama kikundi cha watu waliokopa na kisha kutorejesha fedha hizo.
"Hapa naomba nieleweka kwamba awe diwani au mtumishi wa aina gani kama alichukua fedha hizo atazitapika"
Kuhusu mapato ya halmashauri hiyo alisema mwaka 2022/23 halmashauri ilitenga bajeti kukusanya shilingi bilioni 30.5 ,walifanikiwa kukusanya asilimia 99 ya mapato na mwaka huu 2023/24 halmashauri hiyo imelenga kukusanya shilingi bilioni 48.9 ambapo asilimia 70 zitaenda kwenye miradi.
Pia watakamilisha miradi yote,wamebuni miradi inayoingiza fedha kama vitega Uchumi.
Alisema halmashauri itajenga jengo la utawala ghorofa mbili za awali pamoja na ghorofa ya chini kati ya ghorofa sita pamoja na kujenga Kituo cha afya Cha Sokon one ambapo Rais Samia,ameshatoa fedha za Ujenzi huo.
Ends...
0 Comments