Na Joseph Ngilisho Arusha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Mkoani KILIMANJARO , Morice Makoi,ameipongeza serikali ya rais Samia kwa kuruhusu wananchi kuingia bure kwenye maonesho ya kilimo nane nane yanayofanyika kila mwaka kwa kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi jijini Arusha
Makoi ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu, ametoa kauli hiyo wakati akiongea na vyombo vya habari katika viwanja vya Themi Arusha,mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa Halmashauri yake kushika nafasi ya tatu kwa upande wa banda bora kwa Halmashauri za wilaya ,kanda ya kaskazini.
Alisema hatua hiyo imebeba dhana nzima ya tukio la maonesho hayo tofauti na zamani ilionekana kama ni maonesho ya kibiashara zaidi.
"Maonesho ya mwaka huu yamebeba dhana nzima ya maonesho ya kilimo,serikali imetambua umuhimu wa watu wote kuingia bure na kujifunza kila kitu kinacholetwa hapo "
"Nichukue fursa hii kuipongeza serikali chini ya rais Samia Suluhu Hassan na makamu wa rais dkt Philpo Mpango kwa kufikiria na kuamua kufuta viingilio vya maonesho hayo ndio maana mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa ,watu ni wengi sana mwaka huu walioingia"
"Hili jambo watu wengine wanaweza kuona ni dogo lakini katika historia ya nchi hii serikali imeamua kuhakikisha kilimo kinapewa nafasi na wananchi wanashiriki kilimo cha kitaalamu na wanalima na kuzalisha chakula cha kutosha."
"Wananchi walioingia bure wakiwemo ,wanafunzi na vijana na watu wazima ,kila mtu amepata fursa ya kuona na kujifunza jinsi ya kuzalisha mahindi ,mboga za majani mtama na jinsi ya kusimamia mifugo na hii itasaidia kuchochea uchumi"
Katika hatua nyingine aliwashukuru viongozi wenzake kutoka halmashauri hiyo kwa kufanikisha ushindi huo na kuahidi kufanya vizuri zaidi ili kipindi kijacho halmashauri yao iweze kuibuka na ushindi wa namba moja.
Ends..
0 Comments