Na Joseph Ngilisho Arusha
KIKAO cha Uchaguzi cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha,kimemchagua Joseph Abraham Mollel, Diwani wa Kata ya Kimandolu,Jijini Arusha,kuwa Naibu meya baada ya kupata kura zote za ndio.
Abraham anakuwa naibu meya baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi wa ndani ya chama cha Mapinduzi ccm,uliofanyika mwezi Uliopita kwenye Ukumbi wa ccm,Mkoa na kumshinda aliyekuwa Naibu meya kwa vipindi viwili mfululizo Diwani wa Viti maalumu Veronica Mwilange
Kwenye uchaguzi uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Arusha na kushirikisha madiwani wote akiwemo mmoja wa Chadema,alipita bila kupingwa.
Veronica Mwilange,aliyekuwa Naibu meya,aliyemaliza muda wake,wa kipindi cha Miaka miwili na nusu aliwapongeza madiwani na kuwashukuru kwa kumuamini,amewashukuru watumishi wa Jiji kwa ushirikiano,amepongeza meya kwa ushirikiano na madiwani wenzake.
Kwa upande wake Naibu meya mteule,Diwani Abraham Mollel ,alisema anawashukuru madiwani kwa Imani yao kwake ya kumpitisha Kwa kura zote ,amechukua nafasi hiyo kwa nia Moja ya kuwaunganisha madiwani watumishi na Serikali kuu atakuwa mshauri mwema,atashirikia na Diwani mmoja mmoja .
Kikao hicho kimewachagua Wenyeviti wa Kamati mbalimbali ambapo Diwani Doita Issaya,wa Kata ya Ngarenaro,amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Elimu na huduma ya Jamii kwa kipindi cha pili.
Wajumbe wamemchagua Diwani Jacob Meja Mollel,kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji baada ya kupata kura 8 na kuwashinda Mwenyekiti aliyekuwa akitetea kito hicho,Diwani Nabot Silasi aliyepata kura 3 na Diwani Prospal Msofe,akipata kura 4 ,Alex Matin,akipata kura Moja.
Wajumbe wamemchagua Diwani
Michael Kivuyo , kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya maadili huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Diwani ,Mahamoud Omari wa Kata ya Ungalimited,hakugombea.
Akitoa nasaha zake Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Felician Mtahengerwa,amesisitiza halmashauri ikamilishe viporo vya miradi yote Kwa kuwa fedha zipo nyingi na wameshakaa na Wakandarasi wote na wamekubaliana kukamilisha miradi yote ndani ya wakati ikuwemo ujenzi wa hospitali ya Wilaya na jengo la utawala la Jiji .
Alisema kuwa ni aibu kukutana na hoja ya kutokukamilika kwa miradi hiyo na Wamepewa maelekezo ya kukamilisha miradi yote na ahadi zote za Ilani ya chama.
Alisema atahakikisha maelekezo ya Chama yanayotekelezwa miradi yote ukamilike na hataki kusikia fedha za miradi zinarudi wakati miradi haijakamilika ambayo imetengwa na mwaka
Alisema kuwa hayuko tayari kuona mwaka wa fedha unakwisha na fedha zinarejeshwa na matokeo na miradi haijakamilika na matokeo take ni miradi kutekeleza kwa kutegemea fefha za bakaa,
Akiahirisha kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Maximilian Illanghe,ameitaka Kamati ya mipango Elimu na huduma za Jamii,nayoongozwa na Diwani Issaya Doita kuhakikisha halmashauri inajenga na kukamilisha ujenzi wa shule za mchepuo wa Kiingereza
Aidha ameitaka Kamati ya mipango miji ambayo inaongoza na Mwenyekiti mpya Diwani Jacob Meja Mollel,kuhakikisha inadhibiti ujenzi holela ambao umekithiri maeneo mbalimbali ya Jiji
Alisema Kamati hiyo ihakikishe ujenzi holela unakomeshwa wapo wananchi
wanaojenga bila kufuata taratibu na matokeo yake watu wanajenga jolela mpaka mabarabarani hivyo wasimamie
Kuhusu mapato,amewasisitiza madiwani kuhakikisha wanashirikiana na watendaji kukusanya mapato kwenye kata zao sanjari na kusimamia swala zima la usafi haridhishwi na hali ya usafi kwa kuzingatia kuwa Arusha ni mji wa kitalii.
Alisema kuwa Vipaumbele vya halmashauri hiyo ni vitatu ambavyo ni Mapato, hivyo washirikiane pamoja ili halmashauri ipate mapato ya kutosha na miradi itaboreka na posho za madiwani zitaongezeka .
Aliwataka madiwani wasiwagawe wananchi Kwa itikadi zao bali wawaunganishe pamoja Kwa kuwa wao no viongozi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na huduma za Jamii,diwani Doita,amesema mwaka huu wa fedha halmashauri itajenga shule tatu za mchepuo wa Kiingereza Katika kata za Baraa,Lemara na Olmot na mwakani zitaanza rasmi.
Ends...
0 Comments