Na Joseph Ngilisho Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amewapokea madaktari 60 bingwa wa upasuaji wa Nyonga na magoti kutoka nchini Marekani waliotua nchini Kwa ajili ya upasuaji huo Kwa wagonjwa Kutoka maeneo mbalimbali nchini katika hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Mkoani Arusha.
Aidha Madaktari hao ambao wataanza upasuaji Kwa wagonjwa 200 waliojiamdikisha ,wanatarajia agosti 11 hadi 17 mwaka huu kwenye hospital ya Arusha Lutheran Medical Center iliyopo Jijini Arusha (ALMC).
Akizungumza Mara baada ya kuwasili Mkoani Arusha Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha John Mongela Alisema kwamba ujio wa madaktari hao ni Neema kwa watanzania na ni zao la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan baada ya ziara yake nchini Marekani.
Alisema kwamba Rais Samia baada ya kufungua Diplomasia ya Mataifa mbalimbali nchini Sasa imeanza kufunguka hivyo fursa mbalimbali zinaonekana nakuwataka wananchi wote walipata nafasi hiyo ya matibabu kujitokeza kupata huduma hiyo.
Awali Naibu Waziri wa Afya dkt. Godwin Mollel alieleza kwamba madaktari hao wanaenda kumunga mkono Rais wetu na wanaenda kufanyakazi Kwa niaba ya Rais ya kumgusa kila Mtanzania ndio maana umeona hata madaktari wa Ndani wamekuwa wakizunguka kila mahali Kutoa Tiba mbalimbali maeneo ya nchini yetu.
Alisema kuwa ukiona madaktari wanatibu wagonjwa Kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu kama miezi 2 iliyopita madaktari wetu huko Kijiji cha Pohama Singida waliwaona wagonjwa zaidi ya 1500 wengine walitubiwa hapo hapo na madaktari wetu na wengine wamechukuliwa kuja kufanyiwa upasuaji.
“Tiba ya Mgonjwa Moja Ukisema unagharamia matibabu na vifaa na kukaa wodini milioni 28,000 Leo wenzetu Kwa hisani ya Rais wetu madaktari Hawa wanakuja na vifaa vyao madawa Yao kila kitu kinachohitajika haya ndio maboresho unayosikia tunasema unaposikia Rais wetu ni mwanadiplomasia ambaye anazunguka Duniani na kujenga mahusiano na Matunda ndio kama haya”
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi zima la madaktari na matibabu hayo, Lazaro Nyalandu alisema kwamba wamewashauri wadau hao kuona umuhimu wa Kutoa matibabu maeneo mengi ya nchi yetu wafikirie kwenda Mtwara,Lindi Mbeya Iringa Kigoma Tabora Mwanza Shinyanga na Zanzibar .
Alisema adhma ya Rais watahakikisha inatimia ndio maana wagonjwa wengi waliojiandikisha wanatoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania na Kanda ya kaskazini wajue mkono wa mama Upo na wataendelea kuona upendo ambao ni WA dhati na Mama anaendelea kuwashika mkono wale ambao katika hali ya kawaida hawangeweza kumudu gharama za matibabu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Medical Center ALMC Dkt.Goodwel Kivuvyo alisema kwamba wagonjwa wengi wanaokuja kwenye kliniki hiyo ni wa Nyonga na Mifupa ma ujio wa madaktari hao itakuwa ni jambo la msingi Sana Kwani gharama za mgojwa Mmoja ni takribani milioni 28 Kwa upasuaji Moja na zaidi ya bilioni 2 zitatumika Kwa vifaa na matibabu .
Naye kiongozi wa madaktari hao Dkt.Steven Meyer Kutoka Taasisi ya mifupa STEMM amesema ujio wao nchini ni kuunga juhudi za mh.Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kufanyakazi na wenzao Kwa lengo la Kutoa huduma hii ya matibabu Kwa wananchi wa Watanzania Kwani mh.Rais alituonyesha upendo wa dhati alipotembelea Marekani nasi tumeona tumuunge Mkono.
Ends..
0 Comments