Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amepongeza uwekezaji wa kiwanda kipya cha kwanza Tanzania cha kuunganisha vishikwambi na vifaa vya mawasiliano cha Tanztech Electronics ltd kitakachosaidia kuimarisha teknolojia ya mawasiliano nchini .
Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Njiro jijini hapa,wakati wa ziara yake ya kikazi na kusema kwamba ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua moja wapo ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishikwambi katika shule za awali na sekondari.
"Niwapongeze sana kwa uwekezaji huu naimani Vishikwambi mtakavyozalisha vitasaidia mashuleni, kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia Teknolojia ya mawasiliano katika kujifunza mitaala mbalimbali"
Waziri alisema kwamba ndoto ya rais Samia Suluhu ni kuona fursa za uwekezaji katika sekta ya Sayansi na Teknolojia inakuwa na kupiga hatua na kuleta maendeleo kwa Watanzania wengi kuendana na dunia ya kidigitali.
Aidha alimtaka mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho cha Tanzteck Eletronics limited, kuboresha huduma zake na kuanza kuzalisha bidhaa zinazoendana na wakati katika soko la Teknolojia ya sayansi .
Alisema Vishkwambi vitakavyozalishwa visaidie kukidhi mahitaji ya elimu kwa wanafunzi na kutumika katika maofisi na asasi mbali mbali na kwamba serikali iko tayari kusaidia kufikia malengo ya uzalishaji wa Vishkwambi na vifaa vingine vya mawasiliano kama dira yao inavyo onyesha
"Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na imetoa fursa kwa wawekezaji kuja nchini kuwekeza na tupo tayari kushirikiana na mwekezaji kuakikisha kwamba uwekezaji unakua wa tija na mafanikio kwa taifa "
Awali mkurugenzi wa kiwanda hicho, Gurveer Hans alisema kuwa kiwanda hicho kimeanzishwa kwa ushirikiano na watu wa China ambao wana uzoefu mkubwa masuala ya Teknolojia.
Alisema kiwanda hicho ambacho tayari kinausajiri na Uthibitisho kutoka BRELA,TRA,TIC,PPRA,NEMC na TCRA kitakuwa na uwezo wa kuunganisha,Vishkwambi(Tablets),Simu janja(Smart Phones)Komyuta mpakato(laptop),Smart Projectors,WiFi na mini routers na mita za Luku za Umeme.
Alisema vifaa vingine ni Prepaid mira za Maji,Vifaa vya kupima Madaktari (Electronics Stethoscopers na Multi -parameter Health Monitors.
Mkurugenzi alisema kuwa kiwanda hicho kwa sasa kinauwezo wa kuunganisha simu janja (smartphone)zipatazo 40 kwa mwezi ,Vishikwambi 30,000 ,Laptop 15,000 na smart projectors 10,000.
Alisema matarajio ya kiwanda hicho ni kuongeza Teknolojia za kisasa nchini katika masuala ya kidigital kwamba kiwanda hicho kitashirikiana na serikali katika kusambaza Vishikwambi mashuleni kwa gharama nafuu.
"Kuanzisha kwa kiwanda hiki kutaongeza ajira na pia kutapunguza suala la kuagiza bidhaa nje kwa gharama kubwa"
Aliiomba serikali kupunguza ama kuondoa kabisa ushuru wa vifaa wanavyoagiza nje jambo litakalosaidilia kupunguza gharama bidhaa wanazozalisha na hivyo kuwapa unafuu wanafunzi,taasisi na mashirika kumudu gharama.
Ends.....
0 Comments