DIWANI MSANGI AGEUKA LULU KANISANI ,WAUMINI WAPAGAWA WAMSHANGILIA, WAMFUTA MIGUU KWA MIKONO,AWAMWAGIA MAPESA KIBAO

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 

Diwani wa Kata ya Sombetini BAKARI MSANGI leo amegeuka kivutio kwa waumini wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania KKKT usharika wa Sombetini mtaa wa Kirika baada ya kusali nao  pamoja  na kushiriki harambee ya upanuzi wa kanisa hilo ambapo alichangia sh, milioni 1 kati ya milioni 80 zinazohitajika. 

Wengine waliochangia ni waumini wa kanisa hilo kupitia jumuiya zao ambapo jumla ya mchango uliopatikana leo ni zaidi ya milioni 37.

Akiongea mara baada ya kukaribishwa na kiongozi wa kanisa hilo,MSANGI aliwashukuru waumini hao kwa upendo na ukarimu wao na kueleza kuwa amebarikiwa sana katika ibadan hiyo.
"Mchango wangu huu ninaoutoa ni kidogo lakini ndio niliobarikiwa na una maana kubwa katika ujenzi wa nyumba ya mungu na ninaahidi kuendelea kuchangia ujenzi wa kanisa hili hadi likamilike"
 
Hata hivyo wakati akiendelea kuongea kanisa zima liliripuka kwa Shangwe na baadhi yao walishindwa kujizuia na kwenda kumshangilia kwa kumpepea na kumfuta viatu kwa mikono. 


Katika hatua nyingine MSANGI aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuendelea kupiga vita ukatili na kuwataka wazazi kukaa karibu na watoto wao ili kuepusha vitendo vya ubakaji vinavyoendelea kukithiri na kuathiri watoto .

"Siku hizi ubakaji na  ulawiti umekuwa mkubwa sana naombeni
 sana waumini na wazazi wenzangu kuweni karibu na watoto wetu tuwaangalie kwa makini, maana dunia imeharibika.







Ends..





Post a Comment

0 Comments