BREAKING NEWS,MADEREVA BAJAJ WAANDAMANA WAKIILALAMIKIA LATRA,WAFUNGA BARABARA

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Madereva Bajaj  zaidi ya 300 katika jiji la Arusha, wameandamana katika ofisi za Mamlaka ya udhibiti Usafiri, Ardhini  (LATRA) zilizopo katika jengo la MAFAO HOUSE barabara ya kijenge na kufunga barabara hiyo inayotoka kijenge kuingia mjini  na kusababisha msongamano mkubwa wa magari

Madereva hao wanalalamikia hatua ya  kukamatwa ovyo na kutozwa faini huku mamlaka hiyo ikiwanyima lesseni za Usafirishaji katikati ya jiji bila kuwaambia ukweli iwapo hawatakiwi kufanya biashara hiyo.

Hali hiyo imelazimu askari polisi pamoja na askari wa usalama barabarani kufika eneo la tukio ili kusaidia msongamano wa magari ulioibua kero kwa wananchi na wapita njia wa magari.








Post a Comment

0 Comments