BILIONEA WA RUBBY AMJENGEA NYUMBA,AMPATIA GARI MWENYEKITI MSTAAFU,AMPONGEZA CHONGOLO NA RAIS SAMIA,KWA MAENEO YA UCHIMBAJI

Na Joseph Ngilisho,LONGIDO 


Wachimbaji wadogo wa madini ya Rubby katika kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha wameipongeza serikali kwa kuwapatia leseni za Uchimbaji pamoja na maeneo ya uchimbaji hatua ambayo itachochea  maendeleo wilayani humo.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji  wa madini hayo ya Sendeu Agrovet Investment Limited,Gabriel Sendeu Laizer 
wakati  akiongea na wananchi,katika sherehe za kumsimika uchifu ,mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho kuwa chifu wa ukoo wa kipuyo (Laigwanani)ambapo katika hafla hiyo alimzawadia nyumba na gari  vikiwa na thamani ya sh, milioni 40 kutokana na mchango wake wa kuwasaidia maeneo ya uchimbaji

"Nimshukuru pia katibu Mkuu wa taifa wa ccm Daniel Chongolo pamoja na waziri wa madini Dotto Biteko kwakuwa wao wamesaidia sana sisi wananchi wa longido kupewa maeneo haya Kwa ajili ya kufanya kazi hii ya uchimbaji ambayo kwakweli imesaidia sana vijana wengi kupata ajira"alisema Sendeu

Alisema kuwa ni vyema wananchi wa Longido wakaendelea kulinda na kuhifadhi vyema ardhi yao Kwa ajili ya vizazi vijavyo kwani  iwapo wataitumia vibaya watasababisha  watoto watakaozaliwa kukosa Ardhi .

"Niwasihi pia vijana ambao mpo hapa mnaofanya shughuli zenu ikiwemo za uchimbaji madini mtumie fedha hizo vyema Kwa ajili ya maendeleo na sio mmalizie Kwa wanawake  pamoja na kunywa pombe ,mkitumia vyema itawasaidia nyie wenyewe pamoja na vizazi  vyenu pia itamsaidia kuongeza pato lataifa"alisema Sendeu

Pia Sendeu alimshukuru Rais Samia Suluhu Kwa kuwapatia  wananchi  wa wilaya hiyo maeneo Kwa ajili ya kuchimba madini hayo ambapo alisema kuwa maeneo hayo yameweza kuwapatia vijana wengi ajira na kuwaondolea umasikini.

Katika kutambua mchango wa Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji hicho wa kufanya kazi nzuri katika kipindi cha uongozi wake,Sendeu aliweza kumkabidhi nyumba aliyomjengea pamoja na gari aina ya Noar vyote vikiwa na thamani ya sh, milioni 40.

Akitoa shukrani zake mwenyekiti hiyo mstaafu wa Kijiji hicho,  Akwelino Nikeni aliwashukuru sana wananchi Kwa namna walivyotambua mchango wake alioutoa wa kusaidia jamii katika kipindi cha uongozi wake ambapo aliahidi kuendelea kuwapa ushirikiano hata katika kipindi ambacho hayupo katika uongozi.

"Nimshukuru pia Sendeu Kwa kunipa gari hii niahidi tu gari hii mbali na matumizi yangu binafsi pia litatumika kuwasaidia wananchi wa Kijiji hiki na kata hii pindi watakapo kuwa na uhitaji wowote pia nyumba hii itanisaidia kuishi Mimi na familia yangu
"alisema Nikeni

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack  Joseph aliwataka wananchi wa  wilaya ya longido  kushirikiana kutunza udongo wa Tanzania maana hakuna hazina nyingine yoyote iliopo au watakao weza kupata zaidi  ya ardhi.

Alimpongeza Sendeu Kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa kazi kubwa ya mzalendo ni kuajiri vijana bila kuangalia mradi awe ni kijana wa kitanzania huku akimtaka kuendelea kuonyesha watanzania upendo na aendelee kusaidia serikali kuwapatia vijana ajira Kwa ajili ya maendeleo pamoja na taifa Kwa ujumla .


Ends .

Post a Comment

0 Comments