Na Joseph Ngilisho,Arusha
MWENYEKITI wa ushirika wa wachungaji wa kipentekosteTanzania(PPFT) Nchni,askofu Pius Ikongo amemwomba rais Samia kuondoa ukimya kwenye sakata la bandari linaloendelea kwa sasa bali ajitokeze na kutoaa tamko la kufunga mjadala huo.
Aidha amesema kuendelea kukaa kimya kwa rais Samia ni sawa na kuhalalisha mjadala huo usifikie kikomo na kuwafanya watu washindwe kufanya uzalishaji wa kiuchumi na kukalia masuala ya bandari
"Baada ya Rais kutamka kuwa ameamua kunyamaza kimya tunamuomba afunge mjadala huo na wale watakaoendelea kutamka wachukuliwe hatua".
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25 mwaka huu Jijini Arusha, Mwenyekiti wa PPF Taifa,Askofu Ikongo alisema kila mmoja ametoa maoni kuhusu suala la bandari na endapo kunakasoro katika mkataba huo zirekebishwe Kwa maslahi ya nchi.
Alimpongeza Rais Samia kwa kutoa kauli ya kunyamaza kimya lakini aliongeza kwa kusema kuwa kunyamaza kimya huko kunatoa nafasi ya watu wengine kuendelea kujadili ilhali suala hilo limejadiliwa sana basi ifike ukomo wake
"Rais anaponyamaza utulivu unakuwepo na kila mtu ameongea lakini kwasababu Rais ametoa nafasi sipingani nao lakini sasa Rais atamke kwakusema sasa basi amepokea maoni ya kila aliyesema kuhusu bandari sasa iwe mwisho"
Alisema ni vema sasa mjadala ya bandari ufungwe hivyo alimuomba Rais afunge mjadala huo kuonana na Rais kwaajili ya
Alisisitiza kuwa endapo Rais atafunga mjadala huo watakaoendelea kuongea au kuhamasisha maandamano watachukulia hatua zitakzostahiki na wale watakaofanya maandamano ya amani ambayo ni shinikizo na kunatofauti kubwa kati ya maandamano ya amani na kutoa maoni.
Mwisho
0 Comments