ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA DKT PIMA NA WENZAKE WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA,ADONDOSHA CHOZI MAHAKAMANI

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA

Mahakama ya hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa mkurugenzi  wa jiji la Arusha dkt John Pima na wenzake wawili kwenda jela kutumikia kifunga cha miaka 20 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 9 ya uhujumu uchumi .

Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu Saraphina Nsana katika kesi namba 5 ya mwaka 2022 ya uhujumu uchumi.


Wengine waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 kila mmoja ni Mariam Mshana aliyekuwa mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji,  na innosenti Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo hakimu Nsana alisema kuwa mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili imejidhisha pasipo shaka na  ushahidi wa upande wa mashtaka na kuwatia hatiani.

"Kwa kuzingatia ushahidi huo na kwamba kama washtakiwa wanarekodi ya makosa ya jinai ,na utegemezi wa familia mahakama inawahukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja na iwapo kama hamjaridhika na adhabu hiyo nafasi ya kukata rufaa ipo wazi".

Hata hivyo bado Dk. Pima na wenzake wanakabiliwa na kesi nyingine mbali na kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi ,namba tano ya mwaka 2022
Ends....

Post a Comment

0 Comments