NA MWANDISHI WETU TANGA -
Waumini wa dini ya Kiislamu kote dunuani wameaswa kujenga mazoea ya kusoma na kuchambua matukio ya tareekh ili kuweza kujua historia ya Dini yao ya vizazi vyake.
Hayo yameelezwa leo Mkoani Tanga na Mudir wa Muasas Sheikh Shaffi Muhammed Nina wakati wa maandamano ya Maombolezi ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhamad ( S.A.W ) Imam Hussein ( A.S) aliyefariki mwaka wa sitini na moja Hijiria.
Sheikh Shaffi amesema kuna haja ya kusoma na kuchambua tareekh kwa kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu vilikuja vikiwa salama lakini kulingana na siasa za walimwengu wamekuwa wakibadili maneno ya vitabu hivyo ila Qur-an ilisimamiwa vyema na Imam Hussein (A.S) na kubaki Quran kama ilivyoshushwa na Uislamu kubaki kuwa Uislamu
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika siku hii ya Ashura akiwemo kiongozi wa taasisi ya Almustafa Khairiya Sheikh Alli Amari Mwazoa na Shekhat Othmani kwa pamoja wamesema kupitia siku hii Waislamu wanapaswa kujifunza kuwa na umoja na kuacha udhalimu baina yao
Mamia ya Waislamu katika mitaa na vitongoji mbalimbali wilaya ya Tanga Mjini wameshiriki shughuli ya siku ya Ashura ya kukumbuka siku ya kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS), Imam Husain AS aliuawa shahidi kikatili na kinyama katika jangwa la Karbala nchini Iraq akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuongoza mapambano ya kishujaa ya ushindi wa damu mbele ya upanga.
0 Comments