UJUMBE SHEIKH SOMBI MAADHIMISHO YA WASHIA,WANASIASA ELEZENI UKWELI SUALA LA BANDARI,ATAKA IMAMU HUSSEINI AENZIWE KWA KUPINGA UKATILI NA UNYANYASAJI

 Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 


WAUMINI wa madhehebu ya SHIA, katika jiji la Arusha,wameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein,mjukuu wa Mtume Muhamada S.A.W ,kwa kuitaka jamii kupiga vita unyanyasaji, ukatili na mauaji ya kutisha yanayoibuka miongoni mwa jamii na kulichafua Taifa kimataifa.

Aidha walitoa tamko kwa wanasiasa na wanaharakati kuhakikisha  wanawaeleza ukweli watanzania kuhusu sakata la bandari ili  waweze kujua ukweli na kunufaika na rasilimali hiyo badala ya kuwapotosha na wanaunga mkono serikali katika hatua za kuwaletea maendeleo wananchi. 

Hayo yameelezwa na Imamu mkuu wa msikiti wa Zahra mkoa wa Arusha, Sheikh Maulid Hussein Sombi,kwenye maadhimisho ya siku ya Ashura,ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Husseini,aliyeuliwa na utawala dharimu wa Yazid bin Muawiyah,kwenye mji wa Karbala,nchini, Iraq.

Alisisitiza kuwa waumini wa dhehebu la SHIA ,hawataki kuona watu wanaishi katika ugomvi ,matusi bali wanakuwa wakweli na wazuri na wanaishi kwa amani na upendo na kupata huduma muhimu za kijamii iliwemo maji ,na wao wameamua kumuenzi mtume Hussein kwa kuwakumbuka wenye shida na kuwaombea . 


"Sisi SHIA,tunamuunga mkono Rais Samia,katika juhudi zake za Kuwaletea maendeleo wananchi wake ila tunawaomba wanasiasa na wanaharakati kuwaeleza ukweli watanzania kuhusu suala la bandari kuliko kuwapotosha" alisema Imamu Maulid.

Sheikh,Maulid,alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kupinga ukatili,manyanyaso ,uonevu na badala yake kujenga upendo ,mshikamano na umoja bila ubaguzi na wanalaani tukio hilo lakuuawa kikatili kwa Imamu Hussein .

"Tunaiomba serikali na jamii kwa ujumla kudumisha mambo mazuri ili kila mmoja aishi kwa amani na maisha mazuri yenye furaha ili tunufaike na rasilimali za nchi yetu"

Sheikh, Maulid,alisema Imam Hussein aliuawa mwezi mtukufu wa Muharram,siku ya Ashura, akiwa na wafuasi 82 wakiwemo wanawake,watoto,Yatima na wajawazito tukio hilo la kikatili na kinyama, limekuwa ni la kihistoria hivyo kwa mwaka huu wamebeba ujumbe wa kuwataka watu kuwa wakweli na wazuri kwa matendo yao na maneno yao.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu jumuiya ya maridhiano na amani,Abdul Razak Juma alisema maandamano hayo yanalenga kupigania uhuru wa binadamu kwa kupinga unyanyasaji wa kijinsia ,mapenzi wa jinsia moja ,ukatili , mauaji na ubaguzi wa kidini na ukabila.

Akizungumzia suala la bandari alitoa rai kwa wanasiasa wasiingize hisia za kidini katika jambo la kitaifa hususani linalohusu uchumi wa taifa.

Akisisitiza kuwa viongozi wa dini kuepuka kutumiwa na wanasiasa kama daraja la kuhalalisha mambo yao ,nifursa muhimu kukosoa kwa busara .
Naye maalimu wa Chuo cha dini cha Ahlul bait centre,Shekhe Muhamad Hashim,alisema wanaadhimisha kifo cha mjukuu wa mtume Muhamad S.A.W alisema maandamano kama hayo hufanyika kila mwaka duniani kote na wao wanaadhimisha kwa namna ya kusaidia jamii kwa kugawa maji ,vyakula na kuchangia damu

 "Maombolezi haya tunayoyafanya kila mwaka tunashiriki kusaidia huduma za kijamii kwa kugawa maji,vyakula ,kuchagia damu,kuchimba visima,kusomesha watoto na kuwajali yatima ila tunaomba serikali ituunge mkono na itusaidie maana tunapojitolea kwa misaada kama hii tunakumbana na vikwazo"





Ends.

Post a Comment

0 Comments