Katibu mkuu wizara ya Ujenzi , mawasiliano na uchukuzi Zanzibar ,Hadija Hamis Rajab,amesema kuwa shirika la posta Tanzania, limepiga hatua zaidi katika matumizi ya Tehama na biashara mtandao ila lazima liboreshe huduma zake na kukaa kiushindani zaidi duniani.
Ameyasema hayo jijini Arusha ,wakati akifungua kikao kazi cha viongozi wa shirika hilo nchini, kinacholenga kujadili changamoto na mafanikio na kuweka mpango kazi wa mwaka 2023/24 kwa maslahi mapana ya taifa.
Katibu mkuu huyo alisema wanajivunia kuona shirika hilo likipiga hatua tofauti na miaka ya nyuma kutokana na matumizi ya biashara mtandao na kuwataka wananchi kuliamini shirika lao ambalo limerahisisha shughuli za uchukuzi na usafirishaji.
"Kwa mabadiliko tulionayo sasa ya kiuchumi,kiasiana na kijamii kama hatutayapa kipaumnele matumizi ya Tehama, tunaweza kuachwa nyuma na mataifa mengine "
Alisema ushindani ni mkubwa sana duniani kwa mashirika yanayotoa huduma kama posta, hivyo ni lazima shirika hilo hapa nchini lijiweke kwenye ushindani ili kuweze kusonga mbele zaidi .
Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo alisisitiza kuzingatia masuala ya sheria za manunuzi akidai kuwa mara nyingi viongozi wamekosa uadilifu na kusababisha mashirika kama haya kukosa mwelekeo na mengine kufa.
Awali mkuu wa shirika posta Tanzania ,Macrice Mbodo alisema mkutano huo wa siku tatu ni kikao kazi kilichowajumuisha viongozi wa posta Tanzania bara na Visiwani kwa lengo la kufanya tathmini na maboresho ikiwemo kusaini mikataba ya kiutendaji kwa mwaka 2023/24
Alisema shirika la posta Tanzania limedhamiria kupitia mpango wake wa nane wa biashara wa miaka minne unaoishia mwaka 2025/26 kulifanya shirika hilo kuwa la mfano wa kuigwa katika bara la Afrika, ukizingatia kwamba makao makuu ya umoja wa posta Afrika (PAPU) yapo Tanzania.
Ends..
0 Comments