Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Meru ,Kennedy Danford Mpumilwa amekabidhi matofari kwa mwenyekiti wa kata ya Shambhalai Burka,ZAKAYO MOLLEL ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kisasa ya chama cha Mapinduzi CCM katika kata hiyo.
MPUMILWA amekuwa alishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha masuala ya utalii.
Akiongea wakati akikabidhi msaada huo,katibu mwenezi huyo alisema msaada huo umelenga ujenzi wa ofisi ya ccm na aliwataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha matofari hayo yanatumika ilivyokusudiwa,katika ujenzi wa ofisi ya chama na sio vinginevyo.
"Tunamshukuru sana katibu mwenezi wa wilaya ya MERU kwa kutusaidia matofari ya ujenzi wa ofisi kwa kweli ni jambo zuri na amekuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya wanaMERU"alisema mwenyekiti ZAKAYO
0 Comments