MKE ACHOMA NYUMBA YA MUMEWE NA KUTOWEKA, ,ALICHUKUA KWANZA VITU VYA THAMANI NA KULIPUA,AMEOLEWA MARA SABA HUYO MUME NI WA NANE,MUME AANGUA KILIO UWIII

 Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 

Balozi wa nyumba kumi ,katika mtaa la Ngusero,jijini Arusha,Joseph Mtinangi,amekosa mahala pa kuishi mara baada ya mke wake kulipua kwa moto nyumba yake na kisha kutoweka kusikojulikana huku sababu zikiwa bado hazijulikani.

Akisimulia mkasa huo kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi,Mtinangi ambaye ni mume wa nane kuoa mwanamke huyo,alisema kuwa siku ya tukio majira ya jioni alipata taarifa kuwa nyumba yake inateketea kwa moto na alipofika alikuta moshi mkubwa umetanda ndani ya nyumba na majirani wakisaidia kuzima.
Mume.
Mke 
Alisema alifanikiwa kuingia ndani ya nyumba na kukuta mtungi mdogo wa gesi ukiwa umefunguliwa unatoa gesi, huku moto ukiendelea kuwaka katika chumba cha kulala .

Balozi hiyo alimtuhumu mke wake kuchoma nyumba yake na kabla Ya kutelekeza tukio hilo alichukua baadhi ya vitu vya ndani na kutoweka kwa kutumia usafiri wa  pikipiki aliyokuwa amekodisha akiwa amefungaza na vitu mbalimbali.

Alisema alianza kuishi na mwanamke huyo bila ndoa miaka mitatu iliyopita na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja lakini wakati akishi naye balozi huyo alikuwa na watoto wake wawili kutoka kwa mke mwingine ambaye waliachana.

"Nikiwa na mwanamke huyo alikuwa akiwatesa watoto wangu  jambo ambalo liliniumiza sana na kila ninapomuuliza alikuwa mkali na kuibua ugomvi huku akisema nikipata sumu nawawekea"

Balozi huyo alidai kuwa mkewe alikuwa  na tabia ya kutoroka nyumbani  mara kwa mara na kuiba vitu vya ndani na kwenda kuishi kusikojulikana hata hivyo baadaye hurejea hapo nyumbani na kuomba msamaha.

Alisema mbali ya kuwatesa watoto wake,amekuwa na tabia ya kurejea nyumbani usiku wa manane akiwa amelewa na anapomhoji hudai kuwa alikuwa kwa wanaume mwingine.

Mmoja Ya jirani katika nyumba hiyo,Samweli Laizer alisema majira ya jioni aliona moshi mkubwa  katika nyumba hiyo ya balozi ndipo walipoanza jitihada za kuvunja dirisha ili kuzima moto huo.

Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo ,Emanuel Mboya pamoja na ndugu wa balozi huyo Agness Shaban ,waliiomba Jeshi la polisi nchini kumsaka  mwanamke huyo popote alipo na kuchukulia hatua kali  ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.




Report book(RB)

Ends..



Post a Comment

0 Comments