Na Joseph Ngilisho Arusha
Mamia ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwemo wanafunzi wa shule,wamekumbwa na adha ya usafiri mara baada ya madereva wa daladala Mkoani hapa kugoma kwa kile wanachodai kuwa ni Bajaji kufanya Kazi kama daladala na hivyo kuwalazimu abilia kupanda Guta na kutembea kwa miguu.
Mgomo huo ambao umeanza mapema leo ,umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wamefungua shule leo,ambao walionekana wakiwa kwenye vituo vya usafiri wakisubiri magari mbalimbali na wengine wakilazimika kudandia pikipiki za mizigo( guta )na wengine kutembea kwa mguu umbali mrefu.
Baadhi ya madereva wa daladala eneo la kwa Mirombo walionekana wakicheza mpira huku magari yao ya usafiri wakiwa wameyaficha maeneo mbalimbali wakiwa na madai kwamba hawatapeleka gari barabarani mpaka serikali itoe tamko juu ya utaratibu mpya kati yao na bajaji ambao hautaathiri mapato yao.
"Sisi tunalipa mapato mbalimbali serikalini na tunalipia ruti LATRA ,lakini hizi bajaji hawalipi chochote lakini wanaachwa waingilie ruti zetu ,tunatakiwa kulipa hesabu ya tajiri ,lakini kazi imekuwa ngumu hakuna mapato"alisema
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Kaloleni , Amisa Juma alisema kuwa tangia amekaa barabarani kusubiri usafiri majira ya saa 12 .30 alifajiri hadi saa 3.15 asubuhi alikuwa bado hajapata usafiri na haewewi atafikaje shuleni.
"Magari ya daladala ni usafiri unaoaminika zaidi na bei zake ni elekezi sh, 200 tofauti na bajaji wanatudai sh,500 na mpaka sasa hatujapata usafiri na sielewi tatizo ni nini ,tunaomba serikali iingilie kati maana sisi wanafunzi ndo tunateseka zaidi "
Mmoja ya madereva wa daladala Fatty Maico ,alisema sababu ya daladala kutofanya kazi ni Bajaji kuingilia ruti za daladala,akidai kwamba abilia wamekuwa na tabia ya kupanda daladala kwa kuwa zinajaa mapema .
"Haice inalipa mapato ya sh, 600,000 kwa mwaka ,pia inalipa bima sh,250,000 na inalipa ushuru wa barabara ,lakini bajaj hailipi chochote ndio maana tumeamua kugoma ili kushinikiza swrikali kupanga utaratibu mzuri usioumiza"alisema.
Naye mdau wa maendeleo jiji la Arusha, Hamadi salumu alisema kuwa mgomo huo unachochewa na wanasiasa (hakumtaja)kwa lengo la kujijenga kisiasa na kudgorotesha jitihada za serikali
Alisema wamiliki wa daladala wamekuwa wakitumika vibaya kwa maslahi ya wanasiasa wanaojipambanua kuwa ni watetezi wa wanyonge.
Akizungumzia mgomo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf alisema kuwa utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza.
Alisema kuwa katika ufuatiliaji wamebaini bajaji nyingi ndani ya Jiji la Arusha hazina leseni lakini zinaruhusiwa kufanya kazi tofauti na daladala ambazo zimekuwa zikipigwa faini kila hatua.
Akizungumzia adha hiyo Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela alisema kuwa wamesikia mgomo huo na wanaendelea na taratibu za kushughulika na madai ya madereva hao wa daladala.
"Sisi tumesikia madai yao na tunaendelea kuyafanyia kazi hivyo niwaombe warudi barabarani kuendelea kutoa huduma na tutawapa majibu ya suluhu ya changamoto yao," alisema.
Hata hivyo Mwakalebela amekiri ongezeko la bajaji ndani ya Jiji la Arusha hasa ruti za Sombetini-Ngusero, pia njia ya Majengo, pamoja na ile ya Uswahilini -Dampo ambapo wameanza kuhukua hatua.
Aliongeza kuwa bajaji zipatazo 350 zimesajiriwa na zoezi kufungwa, lakini kwa haraka haraka kuna zaidi ya bajaji 2,000 ambazo zinafanya kazi na kugeuka kero.
Ends..
.
0 Comments