Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
MCHUNGAJI na Mhubiri Maarufu nchini Kenya ,Ezekiel Odero yupo jijini Arusha kwa ajili ya mkutano mkubwa wa Injili utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia kesho ijumaa Julai 14 mwaka huu katika kiwanja cha Shule Ya msingi Ngarenaro na anatarajia kuombea maelfu Ya watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Akiongea na wandishi wa habari jijini juu ya Ujio wa mkutano wake wa kiinjili ,aligoma kuzungumzia masahibu yaliyompata nchini kenya akihusishwa na sakata la mchungaji mwenzake,Paul Makenzie anayeshikiliwa na polisi akihusishwa kusababisha vifo vya raia wa Kenya zaidi ya 300 wasio na hatia ambao walikuwa waumini wake .
"Mahakama yetu Ya kenya imenizuia kuzungumzia hilo ila taifa langu na nchi yangu inafahamu ukweli wa jambo hilo kwa kuwa wapo kwenye uchunguzi"
Aidha Mhubiri huyo ambaye anakanisa lenye uwezo wa kuingiza waumini elfu 45 kwa mkupuo mmoja nchini kenya, ameahidi kusaidia ufadhili wa kukarabati madarasa yenye changamoto katika shule hiyo Ya Ngarenaro baada Ya kubaini kwamba upo ujitaji wa kuboresha shule hiyo.
"Nikija Tanzania na ile shule ambayo iliyonikaribisha bila kunijua na nione haina mabati na niko nafedha, nijukumu langu kama kiongozi wa Kiroho nisaidie hiyo shule bila kuangalia kama mtoto wangu yupo hapo"
"Hatuwezi kuachia maendeleo serikali Peke yake, mimi nikivuka boda na nipate Tanzania , Uganda ama Kongo kuna tatizo na niko na fedha hautanizuia kuisaidia, sababu sijui kesho yangu, aliyenibariki alinipa mkono mrefu nijue kusaidia na sio sifa zenu, hata niwe na mabilioni mangapi nitaacha hapa"
Mchungaji Ezekiel ambaye ni mkazi wa Mombasa nchini Kenya,alisema kuwa amekuja Tanzania ikiwa ni mara yake Ya tatu kufanya mkutano na hiyo ni kwasababu ni taifa analolipenda na watu wake ni wakarimu sana wenye upendo na akikupenda amekupenda kweli na sio unafiki .
Alisema lengo ni kuja kuhubiri injili Ya Yesu kristo juu ya wokivu ,ukombozi , miujiza na ishara peke yake na huo ndio ujumbe wa yesu alioutoa.
Mchungaji Ezekiel aliwaomba wenye Dhambi waachwe waje kanisani ili wabadilike .kanisa langu wanakuja watu wengi sana wenye Dhambi.
Mchungaji Ezekiel alikiri kwamba huduma Ya unabii ni ngumu kwa sababu ni uongo na kweli
Akizungumzia suala la uwekezaji kwa nchi yoyote,alitoa rai kwa serikali, kushirikisha raia wake juu ya uwekezaji wowote,akidai ni hatua nzuri kwa kuhusisha raia wake ambayo itaondoa sintofahamu.
Ends...
0 Comments