Na Joseph Ngilisho Arusha
Mchungaji Maarufu wa kanisa la Newlife nchini Kenya, Ezekiel Odero aliyekuwa afanye mkutano mkubwa wa Injili Jijini Arusha,amezuiwa na polisi kuendelea na mkutano huo,huku sababu zikitajwa kuwa ni kupisha mlipuko wa Ugonjwa wa kuhara.
"Sitisha mkutano wako na usifanye shughuli hiyo Hadi tamko la mlipuko wa Ugonjwa WA kuhara litakapotenguliwa"ilisema sehemu ya barua hiyo kutoka kwa OCD Arusha.
Odero anatajwa kuwa mfuasi wa mhubiri Paul Mackenzie, anayedaiwa kusababisha vifo vya waumini wake zaidi ya 340 nchini Kenya.
Mhubiri Odero akishirikiana na mwenzake Soni Nabii wa Tanzania, waliandaa mkutano huo katika uwanja wa shule ya msingi Ngarenaro uliopewa jina siku tatu za kubadilishwa na Mungu, uliokuwa uanze jana hadi Julai 16.
Waumini wa mch.Ezekiel wakilia kwa uchungu baada ya mkutano kuzuiwaMchungaji Ezekiel Mkazi WA Mombasa Nchini Kenya wiki hii alikuwa afanye mkutano MKUBWA WA Injili katika viwanja vya SHULE ya Msingi Ngarenaro na aliahidi pia kusaidia ukarabati WA SHULE hiyo .
Akiongea mara baada ya kupokea amri hiyo,alisema kuwa Hana kinyongo na zuio Hilo wala serikali ya Tanzania na anashukuru kupewa heshima kwa kuandikiwa barua hiyo juu ya kualifiwa uwepo WA Ugonjwa huo.
"Ninawaomba Radhi wale WOTE waliofika na kulala kwenye uwanja wa MKUTANO inaumiza moyo wangu sana hasa nikikumbuka Yule mama aliyelia pale uwanjani,kumbuka WATU walitoka maeneo ya mbali sana naamini itakuja siku nzuri zaidi"
Mch.Ezekiel aliwahi kuwa na msuguano na SERIKALI ya Kenya akihusishwa na mauaji ya halaiki, ya waumini wasio na hatia zaidi ya 340 yaliyofanywa na mchungaji mwenzake Paul Makenzie.
0 Comments