FAMILIA YA MAREHEMU DIWANI MAARUFU YALIA KUDHULUMIWA ENEO NA JIRANI



Na Joseph Ngilisho MONDULI 


Familia moja ya Marehemu diwani, Abdilah Ally Warsama wakazi wa Makuyuni, wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,imeingia kwenye mgogoro mkali wa kugombea eneo  wakimtuhumu jirani yao,
 Agnes Mswia maarufu, mama Sophia kuvamia eneo lao na kutaka kuwapora  kimabavu .

Mtoto mkubwa wa Marehemu, Rahma Warsama pamoja na mdogo wake Mohamed  Warsama walisema kuwa eneo hilo ni mali yao lililoachwa  na marehemu baba yao aliyefariki mwaka 2012,lakini wakiwa katika hatua ya kuliendelez wameshangaa kukuta mama huyo akimpangishia mfanyabiashara wa mbao anayejenga kibanda kwa ajili ya biashara hiyo.

Awali Rahma alifafanua kuwa kabla ya kifo cha baba yao ambaye alikuwa diwani maarufu kata ya Makuyuni, eneo hilo lilikuwa na mgogoro baina ya marehemu na mtu mwingine lakini mgogoro huo ulimalizika na marehemu baba yao kukabidhiwa eneo hilo kisheria.

Alisema baadaye baba yao ambaye alikuwa diwani wa kata ya Makuyuni, mwaka 2012 alifariki dunia na wao kama familia waliamua kusimamia mali za marehemu likiweno eneo hilo lenye ukubwa wa robo ekari.

"Baada ya mzee kufariki chokochoto kuhusu eneo hilo ziliibuka baada ya mama huyo kudai ni mali yake na kuanza kupangisha watu ,na jana tumekuta kibanda kimejengwa kinyume na utaratibu "alisema Mohamed 

Familia hiyo imeiomba serikali kuingilia kati ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kutokea kwani mama huyo amekuwa akitumia mabavu na fedha zake kurubuni viongozi wa ngazi mbalimbali na kusababisha mgogoro huo kutomalizika. 

Naye mwenyekiti wa ccm wa kitongoji cha Simangori Makuyuni,Hasan Ally  alisema kuwa eneo hilo ni mali ya marehemu Abdilah Warsama tangu kipindi akiwa diwani,na baada ya kufariki familia yake ndo wamekuwa wakisimamia mali zake likiweno eneo hilo ila ameshangazwa kuona jirani yake na marehemu akidai ni eneo lake.

"Mimi kama kiongozi na mkazi wa muda mrefu katika ebwo hili ninajua eneo hilo ni mali ya familia ya Warsama sasa huyu mama nimeshangaa kusikia akidai ni mali yake"

Akihojiwa kwa njia ya simu , Agnes Mswia maarufu mama Sophia alisema eneo hilo ni mali yake na alilipata mwaka 1994 kutoka kwa rafiki yake.

Hata hivyo alipobanwa zaidi  alibadilusha kauli yake na kusema kuwa aligawiwa na kijiji mwaka huo 1994 na ana nyaraka zote za umiliki.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Makuyuni,Setty Onaa alipoulizwa alisema kuwa amepata malalamiko juu ya mgogoro huo na ameandika barua ya kuwataka wahusika kufika ofisini kwake wiki hii wakiwa na nyaraka sahihi za umiliki pamoja na mashahidi wao.

Ends  ...

 


Post a Comment

0 Comments