EWURA:TANZANIA SOKO LA NISHATI YA MAFUTA NI RAHISI KULIKO NCHI ZINGINE

 Na Joseph  Ngilisho, Arusha


Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti  wa maji na nishati ,EWURA nchini Dkt.James Andilile amesema Tanzania ni nchi pekee katika nchi za Afrika  mashariki inayouza nishati ya mafuta kwa  gharama ndogo na hiyo ni kutokana na sera nzuri ya serikali katika kujali uchumi wa wananchi wake .

Dkt Andilile alibainisha hayo katika kikao cha nchi zinazounda umoja wa mamlaka ya udhibiti wa nishati Afrika (EREA) kinacho husisha nchi 5, chenye lengo la kufanya tathmini na mipango kwa mwaka wa fedha 2023/24 kuhusiana na shughuli zake za kiutendaji.

Pia alisema kikao hicho kitaangazia madhumuni ya kuweka uwiano wa masuala ya udhibiti kisheria,kikanuni wa kikanda ili kuchochea uwekezaji katika sekta za Nishati kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa jamii.

"Washiriki wa mkutano huu ni Wenyeviti wa bodi za wakurugenzi , Wakurugenzi watendaji na Wataalamu wa Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa masuala ya Nishati Afrika Mashariki EREA kutoka  Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na Tanzania " 


Aidha Dkt.Andilile alisema Umoja huo umekuwa ukikutana mara mbili kwa mwaka ambapo amesema kwa mwaka huu ambao nchi ya Tanzania wakiwa wenyekiti wa Umoja huo chini ya Prof.Marck Mwandosiya kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa EREA,Tanzania imeweza kupata mafanikio katika mambo 3 ikiweko ukamilishaji wa usajiri wa EREA kupitia mamlaka zilizopo nchini.


Aliongeza kuwa mafanikio mengine ni upataji wa ardhi ya hekari 5 katika Mkoani Arusha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kudumu za Umoja huo pamoja na chuo ambacho kitakuwa kikitoa mafunzo kwa wadhibiti katika Kanda ya Afrika Mashariki pamoja na kuwezesha kuanza kwa utoaji wa mafunzo ya kiudhibiti kwa watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wataalamu kutoka Tanzania.


Alisema kikao hicho kitatoa fursa kwa wenyeviti hao kufanya maamuzi ya utekelezaji katika mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema pamoja na uwepo wa ofisi hiyo nchi itaweza kunufaika kutokana na uwepo wa watu ambao watafika kupatiwa mafunzo na kutoa fedha sambamba na kutolewa kwa ajira


Akizungumzia upandaji wa bei ya mafuta Dkt.Andilile alisema nchi ya Tanzania ndiyo nchi ambayo bei ya mafuta ipo chini ikilinganisha na nchi nyingine kwani suala hilo ni sera ya serikali katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi wake na anafurahi kuona imekuwa kimbilio kwa nchi jirani kununua mafuta Tanzania. 

Ends. 

Post a Comment

0 Comments