DIWANI AMWAGA MASHUKA NA BLANKETI KIBAO HOSPITALI YA SERIKALI,ASEMA HUU NI MWANZO MISAADA ZAIDI KUMWAGIKA

 
 
.
Na Joseph Ngilisho Arusha 

 Diwani wa Kata ya Mjini Kati jijini Arusha, Abdu Tojo ametoa msaada ya Blanketi na Mashuka katika kituo cha Afya cha Kaloleni ili kuwasaidia akina mama wajawazito na watoto wanaozaliwa katika hospitali hiyo.


Akikabidhi msaada huo kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya,Dkt Anna Kimaro alisema ameguswa na mahitaji ya hospitali hiyo hasa kwa akina mama wanaojifungua  kwa upasuaji na kuamua kutoa msaada huo .

"Hiki ni kituo cha afya lakini huduma zinazotolewa hapa ni za kiwango cha hospitali na mahitaji ni mengi kutokana na wingi wa wagonjwa wabaokuja kuhitaji huduma Ya afya kwa sababu kipo katikati ya jiji la Arusha "


Alisema msaada huo wa blanketi 56 na mashuka 18 umetokana na jitihada zake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na haukulenga  kujijenga kisiasa bali ni wajibu wake kama diwani kupunguza changamoto zinaIoikabili  hospitali hiyo ili iwe bora na kimbilio la wananchi. 

"Nimeamua kutoa sadaka hii si kwa aababu za kisiasa bali ni wajibu wangu kama diwani kusaidia hospitali hii, namshukuru sana rais Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu ya maendeleo katika kuleta fedha katika hospitali hii iliyopo kata ya kaloleni, lakini inahudumia wananchi wangu wa kata ya kati na maeneo mengine "


Kwa upande wake kaimu  mganga mkuu jiji la Arusha,dkt  Baraka Mundhe alimshukuru diwani huyo kwani mahitaji katika hospitali hiyo ni mengi, lakini msaada huo utasaidia kupunguza changamito zilizopo.

Aidha aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa usimamizi unaofanya hospitali hiyo kuonekana bora na kimbilio la akina mama kujifungua pamoja na huduma zingine,alitoa rai kwa wasimamizi wengine wa vituo vya afya kuja kujifunza hapo.


Awali mganga mfawidhi wa Hospital hiyo dkt Ana Kimaro alimshukuru diwani huyo pamoja na wadau wengine waoendelea kuisaismdia hospitali hiyo.

Alisema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje wapatao 250 hadi 300 kwa siku huku wanaolazwa wakifikia 30 kwa siku, jambo ambalo linahitaji uwekezaji zaidi wa nyezo za kuwahudumia.


"Uhitaji hapa ni mkubwa na huu msaada usiwe mwisho uwe chachu kwa wengine wanaoguswa kutusaidia ,mahitaji ni mengi kwa akina mama wanaojifungua ambao hawana uwezo "

Ends...












.









Post a Comment

0 Comments